Kwa hili la umri Simba wamepiga bao

Muktasari:

MASHABIKI wa Simba na Yanga wamezoeleka kutupiana vijembe kuhusu umri wa wachezaji. Utasikia “jamaa wamesajili wazee, ooh!! Ile ni timu ya wazee, sasa yule si anacheza na wajukuu zake kabisa.” Hayo ni maneno ya kawaida kwa watani hao wa jadi na hakuna upande ambao unaweza kukubali kushindwa kirahisi vita hiyo ya maneno.

MASHABIKI wa Simba na Yanga wamezoeleka kutupiana vijembe kuhusu umri wa wachezaji. Utasikia “jamaa wamesajili wazee, ooh!! Ile ni timu ya wazee, sasa yule si anacheza na wajukuu zake kabisa.” Hayo ni maneno ya kawaida kwa watani hao wa jadi na hakuna upande ambao unaweza kukubali kushindwa kirahisi vita hiyo ya maneno. Hata hivi karibuni baada ya Yanga kumtangaza winga Said ‘Saido’ Ntibazonkiza kujiunga nao kwa mkataba wa miaka mwili, fasta mitandaoni kulichafuka kwa kejeli kwamba Jangwani wamesajili veterani.

Ila ukweli ni kwamba sakata la umri kwa wachezaji huwa ni pana na kuna makundi mawili, la kwanza ni wenye matumizi sahihi ya umri na la pili hufanya udanganyifu ili kucheza muda mrefu.

Kwa Afrika ishu ya umri kwa wachezaji ni kubwa. Hata hivyo katika Ligi Kuu Bara, takwimu za umri hizi hapa na ni kwa mujibu wa fomu maalumu ambazo klabu kuanzia Ligi Kuu hadi madaraja ya Kwanza na Pili walizijaza kabla ya kuanza kwa msimu ili kupata leseni chini ya TFF.

SIMBA SC

Ukweli ni kwamba Simba ndio wanaoongoza kwa kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kwa timu za Ligi Kuu Bara. Kikosi hicho chenye wachezaji 28, kina wastani wa umri wa miaka 26.9 kwa kila mchezaji. Mshambuliaji Medie Kagere na beki kisiki Pascal Wawa ndio waongoza kila mmoja akiwa na miaka 34, huku golikipa namba tatu Ally Salim akiwa na miaka 20, akiwa ndiye kinda Msimbazi.

Umri wa wachezaji wa Simba: Onyango Joash (27), Mzamiru Yasin (25), Erasto Nyoni (32), Kennedy Juma (26), Aishi Manula (25), Shomari Kapombe (28), John Bocco (31), Jonas Mkude (28). Mohammed Hussein (24), Gadiel Michael (24), Ibrahim Ajibu (24), Ibrahim Ame (27), Miraji Athuman (27), Hassan Dilunga (27), Charles Ilanfya (24), Said Ndemla (24), Beno Kakolanya (26). Wengine ni Muivory Coast, Clatous Chama (29), Gerson Fraga (28), Francis Kahata (28), David Kameta (26), Bernard Morrison (27), Luis Miquissone (25), Chris Mugalu (30) na Bwalya Larry (25).

YANGA SC

Huko Yanga wao wana uwiano wa umri wa miaka 24.2. Viungo Haruna Niyonzima na Zawadi Mauya wakiwa na umri mkubwa wa miaka 32 kila mmoja wakati umri mdogo wakiwa ni kipa Ramadhan Kabwili na beki wa kulia Kibwana Shomari miaka 20 kila mmoja. Wengine ni Carlos Sterio Guimaraes Docarmo (25), Faridi Mussa (24), Michael Sarpong (24), Mukoko Tunombe (24), Tuisila Kisinda (24). Yacouba Songne (28), Feisal Salum (22), Deus Kaseke (26), Abdallah Shaibu (22), Raphael Daud (24), Juma Mahadhi (24), Saidi Juma (24), Ramadhan Kabwili (20) na Bakari Mwamnyeto (23).

Metacha Mnata (22), Mapinduzi Balama (23), Waziri Junior (24),Ditram Nchimbi (23), Adeyun Saleh (24), Paul Godfrey (23), Yassin Mustapha (25), Lamine Moro (26), Abdul-Aziz Makame (24), Farouk Shikhalo (24).

KAGERA SUGAR FC

Kikosi huki kina wastani wa umri wa miaka 24.3 kwa kila mchezaji  na mshambuliaji Hassan Mwaterema akiwa miaka 32 na ndo mkongwe, huku Feisal Hilal na Ally Aman wakiwa wadogo kila mmoja akiwa na miaka 18. Wengine ni Said Kipao (24), Bennedict Tinocco (25), Ramadhan Chalamanda (23), Erick Kyaruzi (24), Hassan Isihaka (26), Ally Mtoni (27), Abdallah Mfuko (27), David Luhende (31), Mwaita Gereza (25), Haroun Mussa (20). Ally Nassoro (25), Swamadu Kasim (24), Abdallah Seseme (28), Mohamed Ibrahim (25), Ally Ramadhani (23), Petter Mwalyanzi (28), Nassoro Kapama (24), Mussa Mossi (28), Jackson Kibirige (26).

Yusuph Mhilu (27), Vitalis Mayanga (21), Hassan Mwaterema (32), Sadat Mohamed (23), Mbaraka Yusuph (22), Dickson Mhilu (20) na Erick Mwijage (19).

BIASHARA UNITED

Biashara United ina wastani wa umri wa miaka 23.3, huku Ramadhan Chombo akiwa ndiye faza na miaka 33 na kinda kikosini akiwa Hassan Mkilindi (19). Wachezaji wengine ni Abdulwaheed Adesola (22), Ambose Awio (26), Christian Zigah (21), James Ssetuba (24), Joseph Zziwa (22), Kilufya Kanfwa (23), Timoth Omwenga (24), Angelo Malima (22),Derick Mussa (24).Abdulmajid Mangalo (22), Lenny Kissu (20), Daniel Mgore (21), Tariq Simba (26), Kauswa Manumbu (22), Ally Mwasomolah (20), Mushta Batozi (24), Mpapi Salum (23), Juma Mpakala  (30), Edson Magoma (20), Hamad Tajiri (25), Omary Nassor (25), Ally Kombo (22), Gerald Mdamu (23), Kelvin Friday (25).

MBEYA CITY

Mbeya City wana wastani wa umri wa miaka 23.1, Emmanuel Membe akiwa mkubwa zaidi na miaka 31, huku Abdrazack Hamza (17) ndiye mdogo kikosini..

Wengine ni Haroun Mandanda (22), Faustino Kamalanda (21), Castor Mhagama (24), Keneth Kunambi (22), Mpoki Mwakinyuke (25), Hassan Mwasapili (27), Baraka Mtafya (24), Rolland Msonjo (22), Juma Shemvuni (24). Samweli Mauru (30), Siraji Juma (21), Samson Madeleke (19), Sylivester Chitembe (24),  Abdul Misiru (23), Edgar Mbembela (22), Taro Joseph (20), Seleman Omary (25)na George Sangija (21). Abasalim Chidiebere (29), Rashid Mchelenga (21), Kelvin Kayongo (23), Kibu Prosper (22), Maliki Kapolo (22), Herbet Lukindo (20), Geofrey Mwashiuya (22), Rehani Kibingu (24).

AZAM FC

Huko Azam FC, wachezaji wao wana wastani wa umri wa miaka 24.3.

Kinda zaidi ni Novatus Dismas (18). Mchezaji mkongwe kikosini ni Agrey Morris (36). Kikosi kamili ni David Kissu (23), Benedict Haule (25), Wilbol Maseke (20) Nicolas Wadada (26), Abdul Omary (21), Bruce Kangwa (32), Abdallah Kheri (24), Oscar Masai (20), Yakubu Mohammed (24).

Charles Emmanuel Lukindo (25),  Daniel Amoah (22), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (28), Mudathir Yahya (24),  Khleffin  Fin (19), Awesu Awesu (23),   Ally Niyonzima (24), Never Tigere (30), Frank Domayo (27). Braison Raphael (24), Ismail Aziz (24), Ayoub Lyanga (22), Andrew  Simchimba (20), Idd Seleman ‘Nado’ (25) ,  Obrey Chirwa (26), Shaaban Chilunda (22), Prince Dube (23), Alain Thierry Akono Akono (24)  na Richard Djod (30).

DODOMA JIJI FC

Dodoma Jiji FC ina wastani wa miaka 25.2. Wachezaji hao ni Hussein Masalanga (28), Emmanuel Mseja (32)  Aron Kalamba (26), Anderson Solomon (21), Abubakar Ngalema (24), Ibrahim Ngecha (29), Mbwana Kibacha (28), Hassan Kapona (21), George Wawa (21). Jukumu Kibanda (26), Augustino Nsata (24) , Justine Omary (26), Rajabu Seif (27), Steven Mgaju (26), Jamal Mtegeta (21), Omary Kanyoro (20), Deus Kigawa (34).

Salmin Hoza (26), Cleophance Mkandala (24), Peter Mapunda (29) , Dickson Ambundo (24), Anuary Jabir (22), Khamis Mcha (31), Santos Thomas (22) , Seif Karie (27) na Michael Joseph Chidyalo  (17).

IHEFU SC

Ndani ya Ihefu SC mchezaji mdogo zaidi ni Geoffrey Kitenga (17). Kikosi hicho kina  kina wastani wa miaka 23.2. Wengine ni Andrew Kayuni (27), Isihaka Joseph (23) Alex Venance (32), Mando Mkumbwa (24), Omary Kindamba (25), Eliah Salingo (25), Emanuel Kichiba (25), Michael Masinda (25), Geoffrey Rafael (31), Alen Merere (24).

Wema  Sadoki (21), Sudi Mlindwa (27), Samwel Onditi (18), Omary Hamis (21), John Mbise (22), Willy Mgaya (24), Daniel Jeremiah (21), Abdi Kassimu (22), Enoc Jiah (21), Joseph Kinyozi (28), Omary Mponda (25). Malulu Thomas (26),Issa Ally (21) , Cyprian Kipenye (18), Tepsi Evans (18), Geoffrey Kitenga (17), Paul Luyungu (21)   na Jordan John (18).

TANZANIA PRISON FC

Wajelajela hao msimu huu wametambulisha kikosi chenye wachezaji 26, chini ya kocha mkongwe Salum Mayanga wakiwa na wastani wa umri wa miaka 26. 6 kwa kila mchezaji. Mchezaji mkubwa ni beki Lauren Mpalile (35), huku kiungo Marco Mhilu (19) akiwa ndiye kinda kikosini chenye makazi mjini Sumbawanga kwa sasa baada ya kuhama Jijini Mbeya. Wachezaji wengine ni Jeremiah Kisubi (31), Prosper Kaini (27), Andrew Ntala (34), Michael Ismail (28), Lauren Mpalile (35), Vedastus Mwihambi (22), Benjamin Asukile(32), Nurdin Chona (28), Nikodem Mwaipaja (20).

Dotto Shaban (27), Steve Mwaiajala (23), Jumanne Elfadhili (30), Ezekiel Mwashilindi (21), Lambert Sabiyanga (27), Adilly Buha (23), Marco Mhilu (19) na France Joel (31).

Wengine ni Salumu Kimenya (33), Samson Mbangula (25), Salum Bosco (27), Mohamed Mkopi ((27), Kassim Mdoe (23), Gaspar Mwaipasi (24), Ramadhan Ibata (25), Shedrack Thomas (19) na Jeremiah Juma (31).

GWAMBINA FC

Timu hii imepanda daraja msimu huu yenye maskani yake wilayani Misungwi mkoani Mwanza ina wachezaji 28, na wastani wa umri ni miaka 24. 8 kwa kila mchezaji.

Antony Matogoro (34) ndiye mwenye umri mkubwa kikosini wakati Mohammed Hussein mwenye miaka 20 ndiye mdogo kuliko wote kama inavyoonekana Chini - Mohamed Makaka (27), Isihaka Ibrahim (20) na Sitali Nyambe (25).

Wengine ni Mohamed Hussein (20), Baraka Mtuwi (25), Salum Kipaga (26), Revocas Richard (28), Hamad Nassoro (21), Lameck Chamkaga (26), Novart Lufunga (30), Anthony Matogolo (34), Aron Lulambo (26) na Amos Kadikilo (22).

Gustapha Lunkombi (20), Bilal Abdi (25), Yusuph Kagoma (24), Yusuf Dunia (22), Salim Sheshe (21), Rajab Athuman (26), Jimmyson Steven (21), Said Mkangu (28), Jacob Masawe (31), Meshack Abraham (25), Kapama Abdallah (20), Paul Nonga (32), Japhet Mayunga (26), Miraji Salehe (25) na Morice Mahela (21).

KMC

Hao Kino Boys kikosi chao ambacho mkongwe ni Juma Kaseja mwenye miaka 35, kina wastani wa miaka 24.3 na mchezaji kinda zaidi ni Martin Kigi mwenye miaka 19. Huo ni usajili mpya akiwa ametokea Alliance FC ya Mwanza. Kikosi kamili cha KMC kinaundwa na Rahim Sheikh (21), Juma Kaseja (35), Isra Mwenda (21), David Bryson (22), Andrew Vicent (27), Hassan Kaparata (22), Hassan Kabunda (23), Cliff Buyoya (21), Kenny Ally (28), Paul Peter (21). Emmanuel Mvuyekure (27), Abdul Hillary (27), Denis Richard (23), Kelvin Kijiri (20), Ally Ramadhan (21), David Mwasa (26) na Mohamed Samata (32). Wengine ni Keneth Masumbuko (28), Masoud Abdallah (23), Sudi Abdallah Dondola (27), Ismail Gambo (24), Martin Kigi (19). Lusajo Mwaikenda (20),Reliant Lusajo (24), Jean Mugiraneza (29), Sadala Lipangile (23), Yusuph Ndikumana (27), Salim Aiyee (24) na Samwel Brazio (20).

JKT TANZANIA

Kiungo wa zamani wa Simba na timu ya taifa la Tanzania, Mwinyi Kazimoto na Nurdin Seleman ndio wachezaji wakongwe zaidi kwenye kikosi cha JKT Tanzania ambacho kipo chini ya kocha Abdallah Mohammed ‘Bares’.

Miongoni mwa makinda ambayo yapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na William Mahullu mwenye miaka 18. Kifuatacho ni kikosi kazi cha JKT Tanzania ambacho kina wastani wa miaka 24.6.

Gray Mwankuga (21), Hassan Wahabi (20), Paul Mhidze (29), Jafari Hussein (20), Daniel Lyanga (26), Mohammed Hamis (25), Parick Munthali (27), Michael Pius (30), Hafidhi Mtambo (27) na Nurdin Seleman (32). Wengine ni Anuar Kilemile (23) Klevin Naftal (20), Kelvin Sabato (23). Pia yupo Khomeiny Barwany (23), George Mande (24), Frank Nchimbi (28), Joseph Ilunga (22), Ally Mwale (25), Madenge Madenge (28), Daniel Mecha (26), Richard Maranya (27) Edward Songo (29) na Mgandila Mavumbise (25). Mwinyi Kazimoto (32), Edson Katanga (26), Adam Adam (23), Jabir Ramadhan (22), Said Said (26), Said Luyaya (20) Abubakar Saad (20), Fashano Mtwike (19), Mrisho Daudi (26) na William Mahullu (18).

NAMUNGO FC

Namungo ambao msimu uliopita walionyesha maajabu ikiwa ni msimu wao wa kwanza kushirki Ligi Kuu Bara. Kikosi chao chenye mkongwe Haruna Shamte mwenye miaka 32, kina wastani wa miaka 25.4.

Kikosi kamili cha Namungo na umri wa mchezaji mmojammoja ni kama kifuatavyo: Quansah Joseph (27), Sixtus Sabilo (26), Hashimu Manyama (24), Shiza Kichuya (24), Kalos Kirenge (26), Bigirimana Blaise (30). Adjiguesena Balora (27), Jafari Mohamed (28), Lucas Chembeja (22), Hamisi Swalehe (23), Hamisi Mgunya (25), Iddy Kipagwile (25), Miza Abdallah (23), Rogers Gabriel (24), Abdulhalim Mohamed ‘Gaucho’ (26). Haruna Shamte (32), Lucas Kikoti (25), Fredy Tangalo (23), Jonathan Nahimana (21), Frank Magingi (21), Edward Manyama (26), Nzigamasobo Styve (30), Stephen Duah (26), Stephen Kwame (26) na Amani Kyata (27).

MWADUI FC

Kikosi cha Mwadui hakina mchezaji mwenye umri zaidi ya miaka 30, wakiwa na wachezaji wazawa tu kwenye kikosi chao chenye wastani wa miaka 23.3.

Kikosi kamili ni Fesal Abdallah (25), Issa Issa (22), Raphael Daud (24), Athanas Mdam (22), Fled Songoro (27), Majid Kimbondile (23), Enrick Nkosi (20), Leonard Ernest (25), Pastor Makula (26), Mahmoud Juma (27), Jackson Shiga (23). Issa Yasini (22), Joram Mgeveke (28), James Mganda (24), Mussa Mbisa (22), Halfan Twenye (24), Mussa Mohamed (22), Walace Kiango (21), Salum Chubi (20), Abubakar Kambi (21). Mussa Kanyagha (22), Merickiard Mazellah (22), Msenda Senda (21), Aniseth Revocatus (22), Emanuel Komba (22), Mpokigwa Mwansasu (28), Abasi Kapombe (22) na Obeid Nassoro (27).

RUVU SHOOTING

Ruvu Shooting yenye wakongwe kama vile Juma Nyosso (35) na Fully Maganga (36) ina wastani wa miaka 26.4.

Kikosi kamili na umri wa wachezaji wa Ruvu Shooting ni kama ifuatavyo: Adam Adam (25), Mohammed Juma (25), Emmanuel Martin (23), Abdulrahman Mussa (25), Juma Nyosso (35), Eradius Mfulebe (26), Innocent Simon (26), Cassian Ponera (28) na Abdalla Rashid (26).

Wengine ni Frank Ikobela (24), Issa Kigingi (21), Renatus Kisase (24), Renatus Cosmas (26), Fully Maganga (36), Mau Bofu (29), Bidii Abdallah (27), Ismail Mohamed (27), Kassim Dabi (28), Mose Said (23) na Ayoub Kitala (28). Pia wapo Shaban Msala (22), Kassim Simbaulanga (26), Issa Said (31), Santos Mazengo (21) na Shabani Kisiga (28).

POLISI TANZANIA.

Hawa maafande wenye maskani yao mkoani Kilimanjaro wana kikosi chenye wachezaji 29 na umri wao ni wastani wa miaka 24.9 kwa kila mchezaji. Kipa Green Paul na kiungo Hamad Kambangwa wenye miaka 34 kila mmoja ndio wakongwe kwenye timu hiyo, huku Mshambuliaji Tariq Seif namba zikionyesha ndiye mdogo akiwa na miaka 20. Wengine ni Mohamed Yusuph(28), Peter Manyika (24), Green Paul (34), Shaban Stambuli (31) na Juma Ramadhan (26).

Wengine ni Mohamed Mmanga (28), Lakini Mwakalukwa (32), Mohamed Kassim (24), Iddy Mobby (27), Hussein Rashid (22), Datus Peter (22), Yahaya Mbegu (20), Ibrahim Abdallah (23), AbdulMalik Adam (24), Pato Ngonyani (25), Rashid Juma (22) na Pius Buswita (22).

Pia kuna Hassan Nassor (26), Jimmy Shoji (27), Emmanuel Manyanda (24), Deusdedity Cosmas (21), Erick Msagati (21), Marcel Kaheza (26), George Mpole (25), Ramadhan Kapera (23), Darueshi Saliboko (21), Kilaza Mazoea (21), Tariq Seif (20) na Hamad Kambangwa (34).

MTIBWA SUGAR

Kutoka Turiani, Morogoro, Mtibwa Sugar ina wachezaji 30, ambapo kila mchezaji ana wastani wa umri wa miaka 24. Kinda wao ni Shello Mussa mwenye miaka 16, huku mkongwe akiwa ni beki Dickson Daud mwenye miaka 34.

Wengine ni Aboutwalib Mshery (21), Hassan Kessy (26), Issa Rashid (26), Dickson Job (20), Baraka Majogoro (24), Geofrey Luseke (23), George Makang’a (23), Ally Makarani (24) Kasim Hamis (25) na Jojo Mkele (19). Wengine ni Boban Zirintusa (28), Ibrahim Hilika (25), Jaffar Kibaya (24), Haruna Chanongo (29), Kasim Hamis (25), Shaban Kado (31), Salum Kanoni (31), Mohamed Nduda (31), Razack Ramadhan (19) na Dickson Daud (34).

Pia kuna Shello Mussa (16), Juma Nyangi (21), Riphat Hamis (21), Awadh Salum (24), Salum Kihimbwa (23), Shaban Nditi (28), Aboubakar Ame (21), Onesmo Mayaya (20), Ismail Mhesa (21) na Frank Kahole (18).

COASTAL UNION

Hawa ndio wenye kikosi chenye wastani mdogo wa umri kwa wachezaji wao, wakiwa wamesajili wachezaji 27 - wastani wao ni miaka 22.4 kwa kila mchezaji ambapo Peter Mwangosi na Muhdin Mbuki wenye umri wa miaka 26 kila mmoja ndio wakubwa zaidi wakati kinda wao akiwa ni Hance Msonga mwenye umri wa miaka 19.

Wengine ni Shaban Dunia (22), Yusuph Soka (25), Peter Mwangosi (26), Hassan Kibailo (21), Issa Abushehe (20), Mtenja Albano (25), Muhsini Malima (20), Prosper Aloyce (22) na Seif Yona (20).

Vilevile yupo Haji Ugando (22), Hance Msonga (19), Abubakar Abas (24), Salum Salum (22), Raizin Hafidhi (25), Hassan Makonga (25), Ayoub Masoud (22), Adil Nasor (22), Ayoub Semtawa (23). Rashid Chambo (20), Mwinyi Said, (22), Martin Kazila (24), Idfonce Chegefu (22), Hussein Abel (21) Mudathir Said (22), Muhidin Mbuki (26), Aggrey Ambangile (25) na Hamad Majimengi (21).