Lafargeholcim Tanzania yasaidia mpango wa kukuza uzalishaji wa bidhaa za ndani

Muktasari:

  • Kampuni ya Saruji ya Mbeya (LafargeHolcim Tanzania) ambayo kwa kiasi kikubwa inatambuliwa na chapa yake ya Pozzolanic Lafarge Tembo Cement imeenda mbali zaidi kuisaidia Serikali ya Tanzania katika mpango wa matumizi wa bidhaa za ndani kwa kusambaza bidhaa yake mpya ya Pozzolana kwenye Mradi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere kama bidhaa iliyoleta mageuzi ya kiuchumi ikiwa mbadala wa bidhaa za majivu (fly ash) nchini Tanzania.

Kampuni ya Saruji ya Mbeya (LafargeHolcim Tanzania) ambayo kwa kiasi kikubwa inatambuliwa na chapa yake ya Pozzolanic Lafarge Tembo Cement imeenda mbali zaidi kuisaidia Serikali ya Tanzania katika mpango wa matumizi wa bidhaa za ndani kwa kusambaza bidhaa yake mpya ya Pozzolana kwenye Mradi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere kama bidhaa iliyoleta mageuzi ya kiuchumi ikiwa mbadala wa bidhaa za majivu (fly ash) nchini Tanzania.

Tanzania inaagiza nje fly ash kwa ajili ya matumizi ya sekta ya ujenzi mfano uimarishaji wa barabara na kama kiongeza nguvu cha zege. Fly Ash ni bidhaa baki kutoka kwenye uunguzaji wa makaa ya mawe kwenye mitambo ya kufua umeme.

Kikemikali na kiufundi fly ash na Pozzolana vina asili moja ambayo ni asili ya volkano na saruji. Historia ya matumizi ya Pozzolana kama nyenzo ya ujenzi illianzia miaka ya 500 BC na wagiriki. Lakini warumi ndiyo walianza kuitumia kama mota kwa ajili ya kushikilia mawe kwenye ujenzi na miundombinu mingine iliyojengwa kwenye maeneo yenye maji maji ambayo hadi leo bado ipo ikiwa ni zaidi ya miaka 2000.

Ufanisi wa Pozzolana kutoka sehemu tofauti kwenye ujenzi hutofautiana na hii huamua matumizi yake. Kutokana na bahati ya upekee wa Pozollana inayopatikana Mbeya, Mbeya Cement Company pamoja na kitengo cha utafiti na maendeleo cha LafargeHolcim wamefanikiwa kutafiti matumizi ya Pozzolana iliyosindikwa na yenye nguvu kama mbadala wa Fly Ash.

 Haya ni mafanikio ya kiuchumi na ubunifu kwa sababu inakuza utumiaji wa rasilimali zinazopatikana nchini, vilevile ni uvumbuzi unaolinda mazingira kwa sababu unakuza ujenzi endelevu huku ukihakikisha utunzaji wa mazingira kwa kupunguza Carbondioxide kwenye hewa. Kuanzia mwanzoni mwa Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere mnamo mwaka 2020, LafargeHolcim Tanzania imesambaza pozzolana kwa ajili ya uimarishaji wa barabara na mahandaki ya maji na pia kama kiungo muhimu kwenye uchanaganyaji wa zege ilu kuongezea ubora na nguvu.


Hadi kukamilika kwa mradi huo zaidi ya tani 200,00 za pozzolana zitatumika. Na mradi utakapokamilika umeme utakaozalishwa na bwawa hili utatumika na vizazi vingi vijavyo, siyo tu ndani ya Tanzania bali hadi kwenye nchi jirani. Tembo Pozzolana daima itakuwa sehemu ya furaha ya vizazi hivyo na ukumbusho maana ni suluhisho endelevu kwenye sekta ya ujenzi.