Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lembeli ashtushwa kutoweka kwa mtoto wa dada yake

Muktasari:

Mbunge wa zamani wa Kahama (CCM), James Lembeli amezungumzia taarifa za mtoto wa dada yake,  Raymond Mkulo ambaye tangu  Novemba 18, 2018 hajulikani alipo ikidaiwa kuwa ametekwa na watu wasiojulikana


Kahama. James Lembeli, mbunge wa zamani wa Kahama kwa tiketi ya CCM ameeleza kushtushwa na taarifa za kutekwa kwa mtoto wa dada yake, Raymond Mkulo.

Mkulo anadaiwa kutekwa Novemba 18, 2018 baada ya  gari alilokuwa akiendesha kukodiwa  na watu wasiojulikana katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi mjini Kahama leo Ijumaa Novemba 23, 2018 Lembeli amesema, “Kimsingi nimepokea kwa masikitiko tukio hilo, nimelisikia kwenye mtandao na kulisoma baada ya kutoka Uingereza kweli limenisikitisha.”

“Mkulo hakuwa dereva wangu mimi nilikuwa namtumia kama kijana wa nyumbani lakini jambo lililompata ni baya sana.”

Lembeli amesema mbali na kijana huyo kuwa mwanafunzi wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), mwaka 2005 alikuwa dereva wa mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wakati huo akiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema.

Amesema Mkulo pia amewahi kuwa dereva wa mbunge wa zamani Kigoma Kusini, David Kafulila.