Lissu ampigia debe Dk Hoseah urais TLS

Lissu ampigia debe Dk Hoseah urais TLS

Muktasari:

  • Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amempigia debe mgombea urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Edward Hoseah ambaye ni mkurugenzi mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwamba ndiye mgombea anayefaa kwa sasa. 


Dar es Salaam. Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amempigia debe mgombea urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Edward Hoseah ambaye ni mkurugenzi mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwamba ndiye mgombea anayefaa kwa sasa.

Lissu anayeishi nchini Ubelgiji tangu mwaka 2018 alipokwenda kutibiwa baada ya kushambuliwa risasi, aliwahi kuwa rais wa TLS mwaka 2017.

Katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Lissu amesema Taifa linawategemea wanasheria kupata viongozi watakaozungumza kwa ajili ya taaluma hiyo na utawala wa sheria nchini.

“Tumeitwa tena kuchagua watakaoongoza ofisi yetu. Kama ilivyokuwa hivi karibuni, Taifa letu linatutegemea kupata viongozi watakaozungumza kwa ajili ya taaluma na utawala wa sheria nchini. Wakati huu nampendekeza Dj Eddie Hoseah kama chaguo la rais wetu mpya,” amesema Lissu.

Mbali na Dk Hoseah, wagombea wengine wa urais TLS ni pamoja na Flaviana Charles, Albert Msando na Shehzad Walli na rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stola.