Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani 2022

Saturday August 06 2022
New Content Item (1)

Mkulima, Christopher Dioniz akieleza umuhimu wa kuwekeza katika lishe. Picha na FAO Tanzania.

*Na Tuzie Edwin Ndekia

Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ni maadhimisho ya kila mwaka ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1 hadi 7 Agosti katika nchi zaidi ya 120 ikiwemo Tanzania.

Ni fursa ya kupigia chapuo na ushirikiano na wadau mbalimbali katika kukuza, kulinda na kusaid­ia unyonyeshaji.

Kauli mbiu ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ya mwaka huu, “Ongeza Unyonyeshaji: Elimisha na Saidia,” inatukumbu­sha umuhimu wa kusi­mamia unyonyeshaji na kuhakikisha kuwa wan­awake wanapata taarifa na msaada muhimu

.Maziwa ya mama ni bora

Maziwa ya mama hutoa virutubisho vyote ambavyo mtoto mchan­ga anahitaji katika miezi sita ya kwanza ya mai­sha; huwa kama chanjo ya kwanza kwa watoto wachanga, kuwalinda kutokana na magonjwa na maambukizi mbalimbali.

Advertisement

WHO na UNICEF zinapendekeza kwamba watoto waanze kunyo­nyeshwa ndani ya saa ya kwanza baada ya kuzaliwa, kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa muda wa miezi sita ya maisha (maa­na yake hakuna vyakula au vinywaji vingine vinavyo­tolewa, ikiwa ni pamoja na maji), ikifuatiwa na kuen­delea kunyonyesha hadi miaka miwili au zaidi.

New Content Item (1)

Wanachama wa GIrls Guide Association wakifuatilia katuni za masuala ya lishe. Picha na FAO Tanzania.

Kuanzishwa kwa unyo­nyeshaji kwa wakati ndani ya saa moja baada ya kuza­liwa kunaweza kuzuia asil­imia 22 ya vifo vya watoto wachanga, na kutoa ulinzi mkali dhidi ya aina zote za utapiamlo wa watoto, ikiwa ni pamoja na kupo­teza na kunenepa kupita kiasi.

Watoto ambao hawan­yonyeshwi katika miaka ya kwanza ya maisha wana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kawaida kama vile kuhara, nimonia na pumu, ambayo husababisha idadi kubwa ya vifo vya watoto kila mwaka.

Unyonyeshaji pia hutoa faida za kiafya kwa wanawake kwa sababu husaidia kutenganisha uzazi, hupunguza hatari ya saratani ya matiti na shingo ya kizazi na shin­ikizo la damu, husaidia katika kupona baada ya kuzaa na kupunguza uzi­to, na kunahusishwa na unyogovu mdogo baada ya kuzaa.

Kuvunja vikwazo

Imani ya kwamba kun­yonyesha mtoto maziwa ya mama pekee haitoshi, mila zinazohitaji watoto wachanga kupewa vyakula maalum baada ya kujif­ungua (ili kuwakaribisha duniani), uuzaji wa bid­haa za lishe kwa watoto wachanga, ukosefu wa msaada wa kutosha kwa mzigo mkubwa wa kazi, pamoja na utoaji wa likizo ya uzazi usiotosheleza ni vikwazo kwa akina mama.

Ni muhimu kwa akina mama kuhisi kuungwa mkono na kutiwa moyo na mazingira yao ya kari­bu, ambayo yanajumui­sha wenzi wao, familia, wahudumu wa afya, jamii, waajiri wao na vyombo vya habari, kwa manufaa ya mama na mtoto.

*Ofisa Lishe, UNICEF Tanzania

Advertisement