Madini ya Tanzanite yanavyovutia mauzo ya bidhaa sokoni

New Content Item (3)
Madini ya Tanzanite yanavyovutia mauzo ya bidhaa sokoni

Muktasari:

  • Kampuni  ya kuuza bidhaa mtandaoni ya Q net imeeleza jinsi madini ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania yalivyo na mvuto duniani na kwamba  bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia madini hayo zinakuwa na soko zaidi.

Dar es Salaam. Kampuni  ya kuuza bidhaa mtandaoni ya Q net imeeleza jinsi madini ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania yalivyo na mvuto duniani na kwamba  bidhaa zinazotengenezwa kwa kutumia madini hayo zinakuwa na soko zaidi.

Mtendaji mkuu wa Q net, Malou Caluza amesema saa za Bernhard H Mayer  zinazoundwa kwa madini hayo zinafanya vyema sokoni akibainisha kuwa wanashirikiana na Responsible Jewelry Council (RJC) kuhakikisha bidhaa zote za vito zinapatikana kwa uhalali ili kupunguza uchimbaji wa madini kinyume na sheria.

Caluza amesema utengenezaji huo unaitangaza Tanzania katika sekta ya utalii kupitia madini hayo pamoja na uwepo wa mlima Kilimanjaro.

“Wateja wetu wa kimataifa wamevutiwa na toleo la bidhaa zetu za Timeless Tanzanite collection.  Mapokezi tuliyoyapata yanatia moyo na tunalenga kujipanua zaidi ili kufikia mahitaji na fursa zinazojitokeza.”

“Hakika Tanzanite ni jiwe la kipekee Afrika. Wateja wetu wanaponunua vipande vya mapambo haya ya kifahari, sio tu kwamba wanamiliki vito hivyo vilivyopambwa na mawe halisi yaliyochimbwa kisheria, lakini pia wanasaidia maelfu ya jamii za wachimbaji ambao wanategemea uchimbaji kwa miaka mingi kuendeleza maisha yao,” amesema.