Madiwani Chemba wasimamisha watumishi watano

Saturday May 14 2022
muhimu pic
By Mwandishi Wetu

Chemba. Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoni Dodoma limewasimamisha kazi kwa mwezi mmoja wakuu wa idara ya Mifugo, Sheria, Ununuzi, Utumishi na Elimu Sekondani ili kupisha uchunguzi.

Hatua hiyo imefikiwa jana Ijumaa Mei 13 kufuatia madai ya ubadhirifu wa fedha, kutokufuata sheria pamoja na kutokulinda rasilimali za halmashauri hiyo yaliyoibuliwa katika kikao cha robo ya tatu cha baraza hilo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mwenyekiti wa Baraza hilo Sambala Said amesema kikao hiko kililenga kujadili matumizi ya fedha na kubaini kuwepo kwa ubathirifu.


Ameongeza katika tuhuma hizo ni pamoja na kutokusimamia vizuri vikundi vinavyotakiwa kuchukua mikopopamoja na kutokusimamia masuala ya chanjo vizuri.

“Tumewasimamisha kazi ndani ya siku 30, watumishi wa tano na kuunda timu ya watu wanne kufanya uchunguzi na ukikamilika utaletwa hapa tujue cha kufanya,” amesema Sambala.

Advertisement

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Fatuma Mganga akizungumza katika baraza hilo, amewataka watalamu kuwa na msimamo wa kazi na utalamu hauonekani kwenye vyeti na huku akiileza imani yake kwa wilaya ya chemba kuwa na mafanikio.

Fatuma amesema kila jambo linaloelezwa litazamwe mara tatu tatu na sio kufanya hitimisho ili kutoa tofauti za kugombana kila wakati na madiwani badala ya kuijenga chemba.

Amesema wakati mwingine ugomvi husabaisha matokeo ya kiutendaji kuwa mabaya na kusema hali hiyo ikiendelea ya kutokuelewana kunakwenda kuiosha muda sio mrefu.

Advertisement