Magazeti yaliyofungiwa kuendelea kubaki kifungoni

Wednesday April 07 2021
habaripic
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameelekeza televisheni za mtandaoni tu ndio zifunguliwe na sio vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa sheria.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Jumatano, Aprili 7 2021 na msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa kupitia ukurasa wake wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Samia: Kuna vyombo vya habari mlivifungia, vifungulieni

Ametoa ufafanuzi huo ikiwa imepita siku moja baada ya Rais Samia kuitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa huku akivitaka vyombo hivyo kufuata sheria.

Wadau wa habari wamshukia Dk Abbas, wadai hakumuelewa Rais Samia


Advertisement
Advertisement