Mahakama ya Qadhi yatengua uamuzi kuvunjwa ndoa ya Dk Mwaka

Muktasari:

  • “Baraza la Ulamaa leo tarehe 27/01/2023 limekutana kwa dharura kwa ajili ya masuala mbalimbali na miongoni mwa masuala hayo ni kadhia iliyotokea hivi karibuni katika Ofisi ya Qadhi ya Mkoa wa Dar es Salaam. Kadhia ambayo inamuhusu Dk Mwaka na mkewe Queen.”

Baraza la Ulamaa limetengua uamuzi wa Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam iliyovunja ndoa ya Juma Mwaka aka Dk Mwaka na mkewe, Queen Masanja ikieleza uamuzi huo ni batili.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo ilisema, “Baraza la Ulamaa leo tarehe 27/01/2023 limekutana kwa dharura kwa ajili ya masuala mbalimbali na miongoni mwa masuala hayo ni kadhia iliyotokea hivi karibuni katika Ofisi ya Qadhi ya Mkoa wa Dar es Salaam. Kadhia ambayo inamuhusu Dk Mwaka na mkewe Queen.”

“Ndoa ya bwana Juma Mwaka Juma ‘Dr Mwaka’ na Mkewe Bi Qeenie Oscar Masanja haijavunjika na kwa hivyo kwa kuwa kuna malalamiko yaliyopelekwa katika Ofisi yo Qadhi, malalamiko hayo au kesi hiyo iendelee katika ofisi ya Qadhi na Baraza la Ulamaa linafuatilia kwa karibu juu ya namna shauri hilo na mengine yanayoendelea kwa ajili ya kuchunga nidhamu katika Baraza.”

Ndoa hiyo ya mtaalamu wa tiba mbadala, Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja ilivunjwa Jumatano, Januari 25, 2023.

Kikao cha Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Sheikh wa Mkoa, Alhadi Mussa Salum kiliketi kwa dharura na kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka.