Mahojiano ya mawakili, shahidi wa sita kesi ya kina Mbowe haya hapa!
Muktasari:
Jaji Joachim Tiganga kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi iliyokuwa ikiendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Dar es Salaam. Jaji Joachim Tiganga kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi iliyokuwa ikiendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Jaji Tiganga ameahirisha kesi hiyo baada ya shahidi wa sita wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi na kuhojiwa na mawakili wa upande wa utetezi.
Leo Alhamisi Novemba 4, 2021 mahakama hiyo imepokea ushahidi wa upande wa mashtaka kutoka kwa shahidi wa sita.
Hapa ni sehemu ya mahojiano ya mawakili wa utetezi na shahidi huyo wa upande wa mashtaka
Baada ya kesi kuahirishwa kwa muda kwa mara ya tatu
Mahakama imerejea kwaajili ya upande wa utetezi kumuhoji shahidi
Mawakili wa pande zote mbili wako tayari
Wakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya anaanza kumuhoji shahidi
Wakili: Unakumbuka uliwahi kuandika maelezo polisi kuhusiana na hiki
Shahadi: Ndio
Wakili: Ulikumbuka kuyasoma kukahakikisha ni sahihi
Shahidi: Ndio
Wakili: Unakumbuka ni tarehe ngapi?
Shahidi 23/3/2021
Wakili: Ni muda ulipita
Shahidi: Miezi 11
Wakili: Itakuwa sahihi nikisema wakati unaandika memori yako haikuwa sahihi
Shahidi: Sio sahihi
Wakili: Machi hadi leo miezi saba hukugundua namba ya jalada ilikuwa na tatizo
Shahidi: Nlikuwa naangalia jukumu nililopewa
Wakili: Unataka kusema content ya barua haikuwa na umuhimu
Shahidi: Nlikuwa najali jukumu nililopewa ndio maana nikasema kulikuwa na tatizo la kiuandishi
Wakili: Ulitaja mapungufu ya jalada kwenye barua yako
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: Naomba nipatiwe kielelezo halisi shahidi aweze kujikumbusha.
Wakili: Angalia hayo kama ni maelezo yako uliyoandika polisi
Shahidi: Ndio yenyewe
Wakili: Hebu Soma tusikie kama kuna maneno uliyosema
Shahidi: Katika maelezo hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa
Wakili: Mwambie Jaji kama kuna sehemu yoyote kwenye kwenye maelezo yako
Shahidi: Kwenye maelezo hayapo
Wakili: Ulituonyesha
Shahidi: Utaratibu tukiletewa
Wakili: Ulituonyesha mfumo unavyofanya kazi
Shahidi: Sikuonyeshwa.
Mheshimiwa naomba kuishi hapo
Baada ya Wakili Jeremiah Mtobesya kumaliza kumuhoji shahidi sasa ni Wakili John Malya ameanza kumuuliza shahidi maswali
Wakili: Dhumuni la kufanya usajili wa silaha ni ili kuzuia uhalifu
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Unapofanya uchunguzi kwenye data base yako silaha ambayo haijasajiliwa kuna majibu inaleta
Shahidi: Inasema no record
Wakili: Hizo result umeleta mahakamani leo.
Shahidi: Kile nilichopresent ndio nilicholeta
Wakili: Wakati unaajiunga na Polisi ulikuwa na miaka 24 toka unaajiunga na Polisi umefanya zaidi ya miaka 24
Shahid: Ni sahihi
Wakili: Ulipoletewa uliuliza huenda ina tuhuma au la
Shahidi: Sikuuliza.
Wakili: Ni sahihi kili kilichosajiliwa ndio unachofanyia uchunguzi
Shahidi: Kama itakuwa imeingizwa kwenye mfumo
Wakili: Kwenye mazingira kama haya utajuaje kama namba zimefutwa
Wakili: Aina ya Silaha na mtengenezaji ndio tunaangalia
Shahidi: Kama zimefutwa nazo
Shahidi: Tunaangalia zile parameter tatu
Wakili: Umewahi kukutana na mazingira kama namba zimefojiwa
Shahidi: Tunaangalia zile
Wakili: Hiyo bunduki hukuletewa ni sahihi
Shahid: Sikufanya hivyo
Wakili: Unafanya kazi siku ngapi katika wiki
Shahidi: Saa 24 katika siku zote 7 za wiki
Wakili Mallya amemaliza sasa kaanza Wakili Fredrick Khiwelo
Wakili: Ni kweli tarehe 25 ulipokea barua kutoka kwa ASP Msangi
Shahidi: Kweli
Wakili: Mpo wa ngapi kwenye hicho kitengo
Shahidi: Tuopo 20
Wakili: Ulitoa taarifa ya umiliki au uchunguzi
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwa mujibu wa maelezo yako ulitoa nini
Shahidi: Nilisema silaha haijasajiliwa
Wakili: Na wewe ulitakiwa kutoa nini
Shahidi: Inamilikiwa
Wakili: Ni sahihi kwamba mnafanyia uchunguzi siku hiyo hiyo mnapopokea barua
Shahidi: Ndio
Wakili: Wewe ulipokea barua tarehe 25 /11/2020 katoa majibu lini
Shahidi: 15 Machi 2021
Wakili: Ni Muda gani umepita
Shahidi: Miezi 5
Wakili: Je katika majukumu yako ulitaja jukumu lako la kutaja umiliki
Ni hayo tu Mheshimiwa.
Wakili Khiwelo amemaliza kumhoji shahidi na sasa anaanza Wakili Peter Kibatala.
Wakili: Kielelezo cha mashtaka namba 10 umetaja barua ya Tarehe 25 Novemba mwaka 2020 je ni sahihi kwamba barua hii ndiyo chanzo chote cha wewe Kuandika barua
Shahidi: Sahihi
Wakili: Ni sahihi kwamba bila barua hiyo wewe usingeandika hiyo barua
Shahidi: Ndiyo sahihi kabisa
Wakili: Sio kawaida yako kuandika tu barua
Shahidi: Itakuwa
Wakili: Je hiyo Barua iliyokufanya uandike barua umekuja nayo
Shahidi: Sikuja nayo
Wakili: Kwa ufahamu wako wewe ni muhimu au siyo huhimu
Shahidi: Kwa upande wangu sikuona umuhimu wa kuja nayo
Wakili: Kwa hiyo barua ndimo ambapo tungepata details za hiyo bunduki ambayo wewe ulipswa uifanyie uchunguzi
Shahidi: Sahihi kabisa
Wakili: Na Ndiyo humo tungeona Namba CZ 100, Callibre 9mm hatuwezi kuona popote zaidi ya hiyo barua
Shahidi: Sahihi kabisa
Wakili: Hujazungumza kabisa kuhusu CZ 100 9mm za ulikuwa unachunguza kwenye hiyo barua uliyoandikiwa na ni sahihi kabisa hujazunhumza kuhusu CZ 100, Callibre 09mm
Shahidi: Sahihi sikuzungumzia
Wakili: Na kuhusu electronic Data Base ulizungumza kuhusu mmiliki wa risasi
Shahidi: Kwenye electronic Data Base inaonyesha kuwa idadi ya risasi za kutumia wakati wa uhai wa leseni
Wakili: Ulitoa maelezo kwa Jaji kwanini hiyo Register hukuleta kama sababu ni nzito au kubwa
Shahidi: Sikutoa
Wakili: Unafahamu kwamba ushahidi wako lazima upitie sehemu kadhaa, Mahakama lazima ipime ushahidi wako
Shahidi: Hiyo nafahamu
Wakili: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji kama ulifafanua kwanini ulishindwa kuleta extract ya negative result
Shahidi: Sikufafanua
Wakili: Nilisikia kwamba kuna typing error kwenye P10
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Sasa Mahakama Itajuaje Kama hakuna tena makosa ya kibinadamu humu?
Shahidi: Ni jukumu la Mahakama sasa kupima
Wakili: Unakubaliana na mimi kuwa akuna kosa linajitegemea kumiliki silaha bila kibali
Wakili: Swali langu la mwisho
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Sheria inaitwaje
Shahidi: Inaitwa sheria ya Umiliki na Udhibiti wa silaha kifungu cha 20
Wakili: Kibatala Mheshimiwa Jaji ni hayo tu.
Wakili wa Serikali Piusi Hilla: Uliulizwa pia kuhusiana na silaha inayoingizwa nchini kutoka nje, wewe maelezo yako hayajaondoa possibility
Shahidi: Mfumo wetu wa silaha na usajili, mfumo wetu unamuimgiza mwishoni kabisa baada ya silaha imeshaingia nchini au kukamilisha utaratibu wa silaha itakwepo Kwenye Lisenced Private Warehouse
Wakili wa Serikali Mheshimiwa Jaji Mimi naishi hapo kam kuna wenzangu waendeleeeee Wakili wa Serikali wezangu na wao hawana
Jaji: Shahidi tunakushukuru unaweza kuendelea
Wakili Kidando: Mheshimiwa Jaji leo tulikuwa na shahidi mmoja tunaomba kuhahiriha shauri hili hadi kesho Novemba 5 saa tatu asubuhi.
Wakili Kibatala hatuna pingamizi Mheshimiwa
Jaji naahirisha kesi hii hadi kesho saa 3 nakuelekeza upande wa mashtaka kuleta mashahidi na washtakiwa wataendelea kubaki chini ya uwangalizi wa Magereza.
High Court iiiiiiiiiiiiii