Majaliwa: Serikali itaendelea kuvitumia vyombo vya habari

Majaliwa: Serikali itaendelea kuvitumia vyombo vya habari

Muktasari:

  • Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango wa vyombo vya habari na itaendelea kuvitumia kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Dodoma. Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango wa vyombo vya habari na itaendelea kuvitumia kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 7, 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Zanzibar alikoshiriki dua ya kumuombea mwaasisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeid Amani Karume.

Mtendaji mkuu huyo wa shughuli za Serikali ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuagiza vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa, kuvitaka vifuate sheria.

Katika maelezo yake Majaliwa amesema vyombo vya habari vilitoa  mchango mkubwa katika msiba na siku 21 za  maombolezo ya kifo cha  rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

"Tutaendelea kushikamana na kuvipa nafasi vyombo vyetu vya habari kwani vimekuwa na mchango mkubwa na Serikali itashirikiana na waandishi kuhabarisha umma," amesema Waziri Mkuu.