Malaria sasa kupimwa kwa vinasaba

Muktasari:

Serikali imezindua maabara ya kwanza itakayokuwa ikifanya utafiti wa ugonjwa wa malaria kwa kutumia vinasaba vya binadamu ambayo, lengo likiwa ni kuwa na ushahidi wa kisayansi katika kupambana na ugonjwa huo.

Dar es Salaam. Serikali imezindua maabara ya kwanza itakayokuwa ikifanya utafiti wa ugonjwa wa malaria kwa kutumia vinasaba vya binadamu ambayo pia itakuwa ikikusanya takwimu zitakazosaidia kufanya uamuzi.
Maabara hiyo imejengwa katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) huku ukifadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melind Gates.
Hilo linafanyika ikiwa ni muendelezo wa jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia azma ya kuutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030.
Akizungunza leo Mei 19 wakati akizindua maabara hiyo, Mganga mkuu wa Serikali Dk Aifello Sichalwe amesema NIMR, Wizara ya afya kupitia mpango wa kudhibiti malaria wakishirkiana na Tamisemi wameendeleza utafiti wa kufuatilia ugonjwa huo na sasa wanataka kutumia mbinu ya vinasaba.
"Lengo ni kwa na ushahidi wa kisayansi katika kupambana na malaria nchini," amesema Dk Sichalwe.
Alisema utafiti huo utaanzia katika mikoa 13 ya Tanzania Bara ambayo inatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria.
"Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma, Kagera, Mtwara, Songwe, Mara, Manyara, Ruvuma, Tanga, Tabora, Njombe,"
alisema utafiti huo pia utasaidia ukusanyaji wa takwimu za vinasaba hapa nchini, kuzichakata na kama wizara itaitumia katika kufanya maamuzi mbalimbali ikiwamo kuandaa miongozo, kutunga sera na kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na ugonjwa huo kwa kutumia ushahidi wa kisayansi.
"Ujenzi wa maabara hii utaongeza msukumo kwenye ufuatiliaji wa magonjwa hasa katika malaria na hatimaye lengo letu la kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030 litafanikiwa." Alisma Dk Sichalwe.
Alisema maabara hiyo inatarajiwa kutumika pia jatika kupima mago jwa mengine ili kuongeza uwezo wa nchi katika kudhibiti magonjwa
"Tumejifunza mengi sna kutokana na ugonjwa wa virusi vya korona, ugonjwa ule ulikuwa mwalimu mzuri sana," alisema Dk Sichalwe.
Katika kupima vinasaba maabara hiyo ni ya nne nchini ila kwa upande wa malaria ni ya kwanza.
Dk Deus Ishengoma ambaye ni Chief Research Scientist kutoka NIMR alisema lengo la kutumia vinasaba kutoka kwa wagonjwa kupima ugonjwa huo ni kutaka kuona kama vimelea vya ugonjwa huo vinatofautiana kati ya eneo moja na lingine nchini
"Pia tuangalie kama vimelea vya ugonjwa huu vinajibadilisha vipi na kama vinaweza kutibiwa na dawa zipi," alisema Ishengoma
Makamu mwenyekiti wa baraza la NIMR, Khadija Malima alisema hadi kukamilika kwa maabara hiyo watu mbalimbali ikiwemo wabia wa ndani pia US Presidents Malaria Initiative (PMI), ofisi ya Shirika la Afya Duniani, Taaisisi za Utafiti, vyuo.
"Tunaimani kuwa maabara hii itaisaidia wizara ya afya katika mpango wake wa kutokomeza malaria na itaisadia pia Tamisemi," amesema Khadija