Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamia wajitokeza kumzika Shirima

Viongozi mbalimbali wa vyama na serikali  wakiwa katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Pius wa X, Tarakea, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ambako ndipo ibada ya mazishi ya kumuaga aliyekuwa mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya shirika la ndege la Precision Air, Michael Ngaleku Shirima inafanyika. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Mamia ya waombolezaji wameendelea kufurika katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Pius X, lililopo Tarakea, Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya shirika la ndege la Precision Air Michael Ngaleku Shirima.

Rombo. Mamia ya waombolezaji wameendelea  kufurika katika kanisa Katoliki la  Mtakatifu Pius X, lililopo Tarakea, Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro kushiriki ibada ya maziko  ya aliyekuwa Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya shirika la ndege la Precision Air Michael Ngaleku Shirima.

Ngaleku alifariki dunia usiku wa Juni 9 mwaka huu katika hospitali ya Aghakan Dar es Salaam alikokuwa amelezwa Juni 8 mwaka huu.

Viongozi mbalimbali wa chama na serikali wameendelea kuwasili katika kanisa hilo akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,  Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi, wafanyakazi wa shirika la ndege la Precision Air pamoja na wadau wengine.

Ngaleku anazikwa leo Juni 15 katika Kijiji Cha Nayeme, kilichopo Tarakea, wilayani Rombo.