Matukio muhimu ya Dk Magufuli yanayobaki kama alama nchini

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli akiangalia nyaraka za uchaguzi Mkuu baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu, Damiani Lubuva. Kushoto ni mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan. Picha na maktaba

Muktasari:

  • Chini ya uongozi wake nidhamu kwa watumishi wa umma inatajwa iliimarika na vita dhidi ya ufisadi vilipata kasi mpya

Juni 4, 2015: Katika Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma, Dk Magufuli alichukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.

Novemba 16, 2015 Dk Magufuli alimteua Dk Tulia Ackson kuwa mbunge na baadaye alichaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano 2015-2020.

Novemba 19, 2015: Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa 11 baada ya Rais John Magufuli kulipendekeza bungeni jina lake na Bunge kuliidhinisha pendekezo hilo.

Novemba 7, 2015 alitangaza kusitisha safari zote za nje ya nchi kwa watumishi wa umma.

Novemba 9, 2015: Alifanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na kuvunja Bodi ya Wakurugenzi ya hospitali hiyo na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk Hussein Kidanto.

Novemba 20, 2015 Majaliwa Kassim Majaliwa aliapishwa kuwa Waziri Mkuu.

Novemba 26, 2015 Dk Magufuli alitangaza kufuta sherehe za maadhimisho ya siku ya Ukimwi na kuagiza kuwa bajeti ya pesa zote zilizotakiwa kwenye sherehe hizo zitumike kununulia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV).

Novemba 27, 2015 alimtumbua Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade.

Desemba 9, 2015 aliwaongoza Watanzania kufanya usafi na kuwataka wajenge utamaduni wa kudumisha usafi huo.

Desemba 10, 2015 siku 35 baada ya kushika kiti cha rais, Magufuli alitangaza Baraza la Mawaziri ambalo kwa sasa lilikuwa na mawaziri 19, ingawa wizara ni 18.

Desemba 16, 2015: Alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea.

Desemba 22, 2015 alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (Rahco), Benhadard Tito

Januari 25, 2016 alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu, na watendaji wengine wa taasisi hiyo.

Februari 15, 2016 aliwateua Dk Asha-Rose Migiro, Mathias Chikawe na Dk Ramadhan Dau kuwa mabalozi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Februari 18, 2016: Alipiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje bila idhini yake.

Aprili 5, 2016: Alisafiri kwenda Rwanda ikiwa ndiyo ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi tangu alipoapishwa kushika wadhifa wa urais.

Aprili 11, 2015: Alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, ikiwa ni muda wa chini ya mwezi mmoja tu tangu kuteuliwa kwake.

Aprili 19, 2015: Alizindua Daraja la NSSF Kigamboni huku akikataa lisiitwe jina lake na badala yake akaagiza liitwe Daraja la Nyerere ili kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Aprili 26, 2016: Alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Ally Simba.

Mei 20, 2016: Alitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Mei 25, 2016: Aliwasimamisha kazi watendaji wakuu wa Kamisheni ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Juni 23, 2016: Alipiga marufuku mikutano ya kisiasa na kusema wanasiasa wasubiri kufanya siasa kwa ushindani mkubwa baada ya miaka mitano, akisema “sasa uchaguzi umeisha” na “nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kutekeleza niliyoahidi.”

Julai 16, 2016: Alimteua Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kupindi cha miaka mitatu

Julai 23, 2016: Alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya mkutano mkuu maalumu kumpa kura zote 2,398 zilizopigwa.

Agosti 1, 2016: Alipiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje na kuagiza ujenzi wa viwanda hapa nchini.

Agosti 11, 2016: Alipiga marufuku operesheni za kuwaondoa wamachinga mijini na badala yake aliziagiza mamlaka husika kuboresha mazingira ya biashara kwa kundi hilo.

Agosti 2016: Alitangaza uteuzi wa Dk Modestus Kapilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Rashid Othman ambaye alistaafu.

Jumatano, Agosti 31, 2016: Alimteua Doto James kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango

Septemba 10, 2016: Ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya Barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara jijini Dar es Salaam ulianza rasmi

Septemba 29, 2016: Alizindua ndege mbili za Serikali zitakazotumiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL

Novemba 4, 2016: Alifanya mahojiano ya kwanza na vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Desemba 7, 2016: Alimwondoa Lawrence Mafuru na kumteua Osward Mashindano kuwa Msajili wa Hazina.

Januari 1, 2017: Alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba na papo hapo kumteua msomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Tito Esau, kukaimu nafasi hiyo

Machi 1, 2017: Alimteua Salma Kikwete, mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kuwa mbunge

Machi 6, 2017: Alitengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Dk Crispin Mpemba

Machi 15, 2017: Alitengua uteuzi na kumsimamisha kazi Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Uledi Mussa

Machi 20, 2017: Alizindua ujenzi wa barabara ya juu ya juu (Ubungo Interchange

Machi 23, 2017: Alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na kumtupa nje Nape Nnauye aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Machi 29, 2017: Aliteua Kamati Maalumu ya kuchunguza aina na viwango vya madini yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi.