Maurel & Prom inasaidia kukuza uchumi wa Tanzania kupitia gesi

Wednesday July 14 2021
mauleapic

Wafanyakazi wa kampuni ya Maurel Prom wakiwa katika picha ya pamoja

Maurel & Prom ni kampuni ya kimataifa ya utafutaji na uchimbaji wa rasilimali mafuta na gesi iliyojijengea heshima kubwa kwa utaalamu na uzoefu wake wa kiuendeshaji, hususan Afrika.

Tangu mwaka 2005, Maurel & Prom imekuwa kampuni ya kwanza kujikita katika uendelezaji wa rasilimali gesi ya Tanzania, ikiwa na dhima ya kutafuta, kugundua, kuendeleza na kuzalisha rasilimali gesi asilia kwa manufaa mapana ya uchumi, ajira na mazingira ya Tanzania.

Shughuli za uchimbaji wa gesi asilia katika eneo la Mnazi Bay, zinazoendeshwa na kampuni hiyo nchini katika hifadhi ya Ruvula iliyopo Kusini mwa mkoa wa Mtwara, zimechangia kiasi kikubwa kuleta mageuzi kutoka kuwa eneo linalozalisha makaa ya mawe na mafuta ya dizeli na sasa kuwa eneo nyeti kwa uzalishaji wa gesi, likihakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na nafuu kwa minajili ya maendeleo ya kiuchumi.

Hatua hii imesababisha uokoaji mkubwa wa fedha katika mahitaji ya umeme kwa Tanzania, na kwa kutokana na ukweli kuwa gesi ni miongoni mwa nishati safi, imesaidia kupunguza usambaaji wa hewa ya ukaa.

mauleapiccc

Leo, kampuni hii inasimama miongoni mwa wadau wakubwa wa sekta ya viwanda nchini, ikizalisha asilimia 45 ya gesi inayotumika kwa uzalishaji wa umeme nchi nzima, ambayo yenyewe inachangia zaidi ya asilimia 50 ya mahitaji ya umeme ya taifa na ikiwa inatumiwa na zaidi ya viwanda vikubwa 40 (viwanda vya kufua umeme, viwanda vya saruji, gesi asilia iliyogandam-izwa nk..) na maeneo mengine, huku ikikadiriwa kunufaisha takriban shughuli 30,000.

Advertisement

Kampuni hiyo ikiongozwa na utamaduni wake uliojikita katika utaalamu wa kiuende-shaji na utendaji kazi mzuri uliochanganywa kwa pamoja na rasilimali za ndani na maarifa, Maurel & Prom Tanzania inaajiri watu waliopo karibu na maeneo wanayoendeshea shughuli zao na wanatekeleza sera yao ya kuzitumia vyema rasilimali za ndani ambayo imejipambanua katika kukuza ujuzi, uelewa katika eneo la maendeleo endelevu na uto-fauti wa kijinsia.

Kampuni hiyo pia imekuwa ikijikita katika kusaidia kuinua uchumi wa jamii kwa kusaidia utolewaji wa elimu, mazingira na huduma za afya endelevu katika maeneo inayoendeshea shughuli zake ya Mnazi Bay, Mtwara na Bigwa, Rufiji na Mafia, Pwani. Kuhusu Maurel & Prom Tanzania

Maurel & Prom Tanzania bado itaendelea kuchangia katika maendeleo ya Tanzania ya baadaye, kwa kuzalisha gesi asilia ya kuaminika, nafuu na inayosambaza hewa ya ukaa kwa kiwango kidogo, na kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi, jambo ambalo imekuwa ikilifanya kwa ufanisi mkubwa kwa miaka 16 iliyopita.

Imeandikwa na Maliki Muunguja, Mwananchi

Advertisement