Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazao yaingiza Sh1.7 trilioni 2022/23

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde (wapili kushoto) akikata utepe kufungua maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani (SUD). Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dk Rashid Chuachua. Picha na Robert Kakwesi

Muktasari:

Kilo 1.8 bilioni za mazao mbalimbali yenye thamani ya Sh1.7 trilioni zimeuzwa  hadi kufikia Machi, 2023 katika mwaka wa fedha 2022/23.

Tabora. Kilo 1.8 bilioni za mazao mbalimbali yenye thamani ya Sh1.7 trilioni zimeuzwa  hadi kufikia Machi, 2023 katika mwaka wa fedha 2022/23.

Akifungua maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani (SUD) Juni 27, 2023 mkoani Tabora, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde ametaja mazao hayo ni tumbaku, korosho, pamba, kahawa na ufuta.

Mazao mengine ni kakao, mkonge, chai, mbaazi, soya, zabibu, miwa na maharage.

Silinde amesema kutokana na mapato yaliyotokana na mazao hayo, yameongeza mzunguko wa fedha sanjali na kuinua uchumi wa maeneo husika na nchi kwa ujumla.

Katika mwaka huo huo wa fedha, amesema hadi April, 2023 Serikali kupitia benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) ilitoa mikopo ya Sh17.05 bilioni kwa vyama vya ushirika vya wafugaji na wavuvi.

Amesema kati ya fedha hizo, Sh13.7 bilioni zilitolewa kwa wazalishaji katika sekta ya uvuvi na kuwa hadi sasa maombi zaidi ya 359 ya mikopo kutoka vyama vya msingi vya wafugaji na wavuvi yamepokelewa TADB na yanafanyiwa uchambuzi kwa kushirikiana na dawati la sekta binafsi lililopo chini ya Wizara aya Mifugo na Uvuvi.

Kuhusu takwimu za wanachama wa Vyama vya Ushirika amesema imeongezeka kutoka wanachama 6.9 milioni Disemba, 2021 hadi wanachama 8.3 milioni kufikia Machi, 2023.

"Ongezeko hilo limetokana na uhamasishaji kuhusu umuhimu wa kujiunga na ushirika na nichukie fursa hii kuwapongeza wanaushirika kwa kazi nzuri mnayofanya,”amesema

Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dk Rashid Chuachua amesema mkoa huo umenufaika na maadhimisho hayo yaliyofanyika mara tatu mfululizo kwani yameongeza ukuaji wa uchumi kwa kipindi chote yanapofanyika.

Amesema hata kama watafanya tena kwa mwaka wa nne mfululizo, mkoa hauna tatizo na utayapokea kwa mikono miwili.