Mbowe awakumbuka kina Mdee

Saturday May 29 2021
mwenyekitichademapic
By Stella Ibengwe

Shinyanga. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema wanawake 19 waliofukuzwa uanachama baada ya kuapishwa kuwa wabunge bila idhini ya chama hicho ni wapambaji baada ya kujengewa msingi mzuri.

Mbowe amesema licha ya kukisaliti chama hicho, bado kina wanachama wengi wanawake wanaoweza kufanya kazi nzuri ya kuijenga Chadema na kuleta mabadiliko makubwa.

mbowepic

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

Wanawake hao 19, akiwemo Halima Mdee walivuliwa uanachama Novemba, 2020 baada ya kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama hicho. Hata hivyo licha ya kufukuzwa uanachama, walikata rufaa katika baraza kuu la chama hicho.

Ameeleza hayo leo Jumamosi Mei 29, 2021 katika kikao cha ndani cha Chadema mkoani Shinyanga huku akigusia katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia 2015 wanachama wa chama hicho walivyopitia wakati mgumu.

Amewataka wanachama kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutetea haki zao ili kupiga hatua zaidi kwani kazi imeanza na inaendelea hadi mwaka 2025.

Advertisement

Halima Mdee, wenzake 18 wavuliwa uanachama Chadema

Advertisement