Mbowe mwenyekiti mpya CCM Ubungo

What you need to know:

Wagombea wanne walioteuliwa kuwania nafasi hiyo ni Lucas Mgonja, Theresia Chihota, William Masanja na Rogati Mbowe.

T:

S:

Mariam Mbwana, Mwananchi mmbwana@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya mgombea mwenzake wa nafasi hiyo Rogati Mbowe kushinda kwa kura 407.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Oktoba 3, 2022, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Galik Ramadhani alisema kura zilizopigwa ni 732 kati ya hizo mbili ziliharibika.

"Rogati Mbowe amepata kura 407, Lucas Mgonja amepata kura 288, William Masanja kura 27 na Theresia Chihota kura nane hivyo napenda kumtangaza Rogati Mbowe kuwa mshindi wa nafasi hiyo,"

Baada ya uchaguzi huo kuisha na matokeo mwenyekiti huyo mpya wa wilaya ya Ubungo aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua na kuwataka kuvunja makundi na kuungana pamoja kukijenga chama.

This page might use cookies if your analytics vendor requires them.