Mbowe na wenzake wafikishwa Mahakamani, Jamhuri kuanza kutoa ushahidi

Wednesday September 15 2021
mahaka,manipiccc

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

By Hadija Jumanne
By James Magai

Dar es Salama. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Septemba 15, 2021 kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.

Mahakama itaanza kupokea ushahidi wa Jamhuri katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Soma zaidi: Boaz, Kingai kizimbani kesi ya Mbowe


Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa, na Mohamed Abdillahi Ling'wenya.

Advertisement

Serikali inawasilishwa na jopo la mawakili nane wakiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, huku washtakiwa wakitetewa na jopo la mawakili 14, likiongozwa na wakili Peter Kibatala.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Yusuph Siyani.Advertisement