Mbunge Hasunga aitaka Serikali kuwaongezea mshahara watumishi wa umma

Wednesday April 14 2021
HASUNGA PC
By Sharon Sauwa

Dodoma. Mbunge wa Vwawa (CCM), Japhet Hasunga ameitaka Serikali kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma ili waweze kuishi maisha mazuri.

Waziri huyo wa zamani wa kilimo ameeleza hayo leo Jumatano Aprili 14,  2021 katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu mwaka wa fedha 2021/22.

Hasunga amesema mahali popote ili uweze kukamilisha jambo lako lazima uwe na watumishi, “zamani tulikuwa tunasema mteja ni mfalme lakini sasa hivi mteja ni namba mbili, wa kwanza ni mtumishi, kumchukulia vizuri mtumishi ndio atafanya wateja waongezeke.”

Huku akieleza jinsi Serikali inavyotekeleza miradi mbalimbali kulingana na ahadi zilizotolewa na CCM kwenye uchaguzi, Hasunga amesema, “sasa tunaingia kuhakikisha watumishi wetu wanapata maslahi mazuri ili wale madaraja yalikuwa hayajapandishwa yapandishwe, mishahara ambayo ilikuwa haijaongezeka..., naiomba Serikali yangu iwatazame hawa watumishi wetu ili waweze kuishi vizuri.”

Advertisement