Mchango wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika sekta ya elimu Tanzania

Mchango wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika sekta ya elimu Tanzania

Muktasari:

Taasisi za fedha ni mion-goni mwa mihimili ya uchumi katika nchi yoyote. Hawa ndiyo waendeshaji wakuu wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, kijamii na kiuchumi.

Taasisi za fedha ni mion-goni mwa mihimili ya uchumi katika nchi yoyote. Hawa ndiyo waendeshaji wakuu wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo, kijamii na kiuchumi.

Kwa Tanzania, taasisi za fedha zimekuwa mhimili katika kushiriki kwenye mambo yenye manufaa na mchango mkubwa kwa jamii kama utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusaidia uboreshaji wa huduma za jamii kama elimu, afya na miundombinu.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC Ltd) ni miongoni mwa taasisi za fedha zinazotoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu kwenye maeneo mbalimbali na ikiwafikia watu wa rika na shughuli mbalimbali nchini.

Mbali na kutoa misaada ya ujenzi wa madarasa na uboreshaji wa miundombinu kwa shule mbalimbali nchini kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali, NBC imeendelea kutoa elimu ya fedha na uendeshaji wa biashara kwa wadau wake mbalimbali ikiwemo mawakala wa huduma zake, wanafunzi, wakulima, wafanyabiashara, wajasiriamali, waajiriwa kupitia pro-gramu maalumu zilizoandaliwa kwa ajili ya makundi haya husika.

Wanafunzi

Benki ya NBC imekuwa ikiendesha programu mbili za elimu zinazowalenga wanafunzi moja kwa moja ambazo ni;

Program ya mafunzo kwa vijana ya ‘NBC Wajibika’

Ni program inayolenga kuwapatia vijana mafunzo, elimu na ujuzi ili kuwawezesha kuingia kwenye soko la ajira wakiwa na uelewa, mtazamo, utayari na uwezo wa kumudu kujisimamia wenyewe katika maisha na ajira.

Aidha mafunzo haya pia yanawasaidia vijana kufanya maamuzi sahihi, kusimamia uhusiano wa kikazi na wengine, fedha zao kwa namna ambayo inaongeza tija na maendeleo na hivyo kubadili mtazamo wao kuhusiana na suala zima la ajira.

Kupitia mafunzo haya wanufaika wanawezeshwa kuona fursa mbalimbali za kujiajiri.Mpango huu wa wajibika wa NBC, unashughulikia kuziba pengo kubwa linalojitokeza kwa vijana pindi wanapohama kutoka kwenye mfumo wa maisha ya uanafunzi kwenda kujitegemea.

Kuziba pengo hili si tu kwamba kutawawezesha kuhamisha fikra kwa usahihi bali pia kutaongeza ufanisi katika shughuli zao tarajiwa.

Mafunzo ya NBC Wajibika hutolewa mtandaoni kupitia tovuti na ana kwa ana katika semina na warsha zinazoratibiwa na NBC katika vyuo na shule za sekondari mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Programu hii imewafikia na kuwanufaisha jumla ya wanafunzi 12,138 katika vyuo vikuu, vyuo na shule za sekondari 50 nchini tangu kuanza kwake mwaka 2016.

Programu ya udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu (NBC Scholarship)

Katika kuendelea kuhakikisha kuwa vijana wasio na uwezo wa kumudu gharama za elimu ya juu, Benki ya NBC inaratibu program ya ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya juu ambao wana uwezo kimasomo lakini wanatoka katika familia zisizo na uwezo wa kifedha.

Mpango huu wa NBC Scholarship, ulianza 2018 na jumla ya wanafunzi 70 kutoka vyuo vya DUCE, MWEKA, CBE na IFM wamenufaika.

Kati ya hao, wanafunzi 45 wamemaliza vyuo kwa ufaulu mzuri na wanafunzi 21 bado wanaendelea na wapo katika mwaka wao wa mwisho kwenye masomo ya shahada ya kwanza.

Akaunti ya wanafunzi ya NBC

NBC kupitia akaunti yake ya wanafunzi (NBC Student Account), inawawezesha wanafunzi kuweka akiba ya fedha zao wawapo chuoni.

Kupitia akaunti hii, mwanafunzi anapata fedha zake kwa wakati, anaweza kuwekewa fedha na yeyote kupitia wakala wa NBC, matawi ya NBC, ATM za NBC zinazopokea fedha au kwa njia ya simu.

Mwanafunzi anaweza kufanya miamala moja kwa moja kutoka kwenye simu yake na pia anapokea taarifa ya miamala inayofanyika kwenye akaunti yake.

Wafanyabiashara/ wajasiriamali

Benki ya NBC kupitia klabu za Biashara za NBC (NBC BClub)

Benki ya NBC inayo klabu ya biashara inayotumika kama jukwaa la kuwakutanisha wateja wa NBC pamoja na taasisi mbalimbali zikiwamo za Serikali na binafsi, kwa lengo la kuwapatia mafunzo, kubadilishana uzoefu na taarifa za biashara, huduma, mchanganuo wa biashara ili kufikia lengo pana zaidi la kufanya biashara kwa pamoja kuzikuza na kuziendeleza.

Lakini pia klabu hizi zinatumika kwa lengo la kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa wanachama wake.

Mpaka sasa, takribani wateja wadogo na wakati (SMEs) zaidi ya 3,900 wamepatiwa mafunzo yaliyohusu uendeshaji wa maghala (kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje), utunzaji taarifa, kodi, fursa mbalimbali za kibiashara na masoko zilizoko ndani na nje ya nchi, ubora wa bidhaa, usajili wa biashara na kampuni, upatikanaji wa leseni mbalimbali za biashara, usimamizi wa biashara na mafunzo yanayohusu namna ambavyo wateja wanaweza kupata mikopo na huduma mbalimbali za kibiashara kutoka katika Benki ya NBC.

Mafunzo haya yanalenga kuwajengea wateja uwezo wa kuziendesha biashara zao kwa faida kwa ajili ya manufaa yao na manufaa ya taifa kwa ujumla. Benki ya NBC kwa kushirikiana na TanTrade, wameweza kuwafikia wanufaika 694 kwa mwaka wa 2020 tu kupitia kliniki za biashara zilizofanyika Dar es Salaam, Simiyu na Geita ambapo ushirikiano huu ulianza tangu mwaka 2018.Kwa mwaka 2021, Benki ya NBC, kupitia klabu hizi, imeweka mikakati mikubwa ya kuwafikia wafanyabiashara wadogo na wakati wengi na kuwapatia mafunzo ya aina mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuwajengea uwezo wa namna ya kuziendesha biashara zao kwa faida.

Mafunzo haya yatalenga makundi mbalimbali ya wafanyabiashara wakiwamo wanawake ambao wameonekana kuwa na mchango mkubwa katika sekta ya biashara ndogo na za kati.Kutoa mafunzo kuhusu namna bora ya usimamizi na uendeshaji wa biashara, umuhimu wa kutunza taarifa za biashara, upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi, bila kusahau mafunzo juu ya fursa za mikopo na huduma za kifedha ambazo wateja wanaweza kuzipata kutoka katika Benki ya NBC Ltd.

Mpango wa Bima ya maisha na elimu

Watu wengi wanaamini kuwa hawahitaji kusumbuka kuwekeza kwa ajili ya elimu ya watoto wao, lakini ukweli ni kwamba hakuna ajuaye kesho. Mpango wa Bima ya Elimu kupitia NBC (Educare), inakuwezesha kuwekeza fedha ambazo zitatumika kuhakikisha kuwa watoto wako wanapata elimu bora bila kusumbuka hata pale inapotokea kwa bahati mzazi au mlezi hayupo tena duniani au amepata ulemavu wa kudumu unaomzuia kufanya shughuli za uzalishaji fedha kwa ajili ya familia.

Mpango huu kwa kupitia Benki ya NBC ni kwa mtu yeyote na unamruhusu mteja kuwekeza kwa kianzio kidogo tu cha Sh 100,000 au zaidi kadri ya uwezo na malengo husika.

Tukiwa kwenye maadhimisho ya siku ya elimu duniani, NBC mnatoa wito gani kwa wateja wenu?

Tunapenda kuwakum-busha wateja kuzingatia umuhimu wa elimu kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha wanawapeleka watoto shule ili kuwapa urithi huu adhimu na wa uhakika.

Katika kuzingatia usawa wa kijinsia tungependa pia kuwakumbusha kutokuwaacha nyuma watoto wa kike kwani wana haki sawa ya kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wa kiume.

Serikali yetu imehakikisha huduma za elimu zinakuwa bora zaidi huku zikitolewa bila malipo kwa ngazi ya msingi hadi sekondari, hivyo basi wazazi na walezi wahakikishe watoto wanapelekwa shule na vilevile kwa kushirikiana na walimu tuhakikishe ufuatiliaji wa maendeleo ya elimu za vijana wetu.

Imeandikwa na Jafari Juma, Mwananchi