Meli iliyobeba tani 5,623 za Sulphur yawasili Mtwara

Muktasari:

  • Meli ya BOSS7 iliyobeba tani 5,623 za Sulphur ya unga leo Ijumaa Juni 24, 2022 imewasili mkoani Mtwara kutoka nchini Uturuki.

  

Mtwara. Meli ya BOSS7 iliyobeba tani 5,623 za Sulphur ya unga leo Ijumaa Juni 24, 2022 imewasili mkoani Mtwara kutoka nchini Uturuki.

Kuingia kwa meli hiyo inafanya jumla ya viuatilifu vilivyoingia nchini kufikia tani 10,170 katika ya 25,000 zilizoagizwa na Serikali.

Shehena hiyo itagawiwa bure kwa wakulima baada ya wiki tatu, ikiwa lengo la kuimarisha kilimo cha zao

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Francis Alfred amesema kuwa ugawaji wa pembejeo hizo utaongeza uzalishaji wa korosho.

"ingawa kwa sasa mchango wa zao hilo katika pato la taifa kwa mwaka ni Sh500 bilioni, matarajio ya ongezeko la uzalishaji yanalenga kufikisha uchangiaji wa Sh1 trilioni kwa kipindi hicho” amesema

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari Mtwara, Norbert Kalembwe amesema kuwa meli hiyo imebeba Sulphur zaidi ya tani 5000.

"Leo tumeshudia ujio wa meli ambayo imebeba viwatilifu ambavyo ni kwa ajili ya upuliziaji katika mikorosho "amesema.