Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfahamu Halima, Mtanzania wa kwanza kuunda chaja ya simu

Halima Abdul Mtanzania wa kwanza kubuni chaja za simu.

Muktasari:

  • Halima amekuwa Mtanzania wa kwanza kubuni chaja za simu zinazolingana na mahitaji ya Tanzania.



Dar es Saalam. Mnamo mwaka wa 2023, Halima Abdul aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kubuni chaja za simu zinazokidhi mahitaji ya mfumo wa umeme nchini Tanzania, mafanikio ambayo yanatokana na uzoefu wa zaidi ya muongo mmoja katika ujasiriamali na bidii isiyokoma.

Safari ya Halima ilianza mwaka 2011 baada ya kuhitimu shule ya sekondari mkoani Mbeya.

Akiwa na Sh300, 000 alizopewa kama zawadi ya kuhitimu, Halima aliamua kuanzisha biashara ndogo ya maktaba ya kukodisha CD, iliyouza pia vifaa vya simu kama chaja na spika za maskioni.

Kutokana na changamoto ya kukosa fedha za kulipia eneo la kibiashara, alimwomba jamaa yake amruhusu kutumia chumba cha nyumbani kwao kama sehemu ya biashara hiyo.

“Haikuwa rahisi, nilijitahidi kusimamia kila kitu mwenyewe, nikijifunza huduma kwa wateja na usimamizi wa bidhaa huku nikiwa kazini,” anakumbuka anapozungumza na The Citizen.

Baada ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Halima alilazimika kufunga maktaba hiyo. Ili kujikimu akiwa masomoni, alihamia kwenye biashara ya kuuza nguo na baadaye alizidi kupata maarifa ya biashara kwa kuuza bidhaa zake jijini Dar es Salaam, hasa katika Soko la Kariakoo.

Mwaka 2020, kwa ushauri wa mpenzi wake, Halima aliamua kubadilisha mwelekeo wa biashara na kuingia kwenye vifaa vya kielektroniki, hasa chaja za simu. Hata hivyo, changamoto kubwa ilijitokeza, kwani wateja walilalamikia chaja hizo kuharibu betri za simu zao.

“Chaja hizi hazikuwa zimeundwa kwa mfumo wa umeme wa Tanzania,” anaeleza. Akiwa na shauku ya kutatua tatizo hili, Halima ambaye pia ni mhandisi wa simu za mkononi alichukua hatua ya kubuni chaja zake mwenyewe zinazolingana na mahitaji ya soko la Tanzania.

Mnamo mwaka 2023, ziara ya kibiashara nchini China ilimkutanisha na mmiliki wa kiwanda aliyemwelewa na kukubali kusaidia kutengeneza chaja hizo. Kwa pamoja walibuni bidhaa aliyoipa jina Mima, chaja iliyoundwa kustahimili mabadiliko ya umeme wa Tanzania.

“Toleo la kwanza la chaja 10,000 za Mima ilikuwa hatua kubwa kwangu,” anasema Halima. “Nilifurahi sana kuona ndoto yangu inakuwa halisi, kwani chaja ambazo zinaendana na mazingira ya ndani huwa na uwezo wa kudumu zaidi.

“Zinaundwa kwa malighafi bora zinazoweza kuhimili matumizi ya mara kwa mara na mabadiliko ya umeme. Hii huokoa gharama za mara kwa mara kwa watumiaji kwa kuwa hawalazimiki kununua chaja mpya kila wakati,” anasema Halima.

Kwa kuangalia mbele, Halima ana mpango wa kuanzisha kiwanda nchini Tanzania ili kuzalisha bidhaa zinazofaa zaidi kwa soko la hapa na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania.


“Nataka kuzalisha hapa nyumbani ili kuhudumia soko kwa ufanisi zaidi na kusaidia uchumi wetu,” anasema.

Wataalamu wa masuala ya teknolojia wanashauri kuwa kwa kuwa na chaja zinazodumu zaidi na zinazofanya kazi kwa ufanisi, watumiaji hawalazimiki kutupa chaja mara kwa mara na hii inapunguza taka za kielektroniki ambazo zina athari mbaya kwa mazingira.

Chaja zinazobuniwa kwa kuzingatia uendelevu zinasaidia kutunza mazingira kwa kupunguza uchafuzi.

Sambamba na hayo, ubunifu wa chaja zinazolingana na mazingira ya Tanzania unachochea uzalishaji wa ndani, kuunda fursa za ajira, na kuimarisha uchumi.

Chaja zinazotengenezwa ndani kwa kuzingatia mahitaji ya ndani zinahamasisha viwanda vya ndani na kusaidia ukuaji wa sekta ya teknolojia nchini.