Mfalme Charles III kukutana na viongozi wa kisiasa, kidini

Muktasari:

  • Mfalme Charles III leo Jumamosi Septemba 10, 2022 atakutana na viongozi wa dini na kisiasa wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Uingereza katika Kasri la Buckingham.

London. Mfalme Charles III leo Jumamosi Septemba 10, 2022 atakutana na viongozi wa dini na kisiasa wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Uingereza katika Kasri la Buckingham.

Taarifa iliyotolewa leo na Kasri hilo imesema pia Mfalme atampokea Askofu Mkuu wa Canterbury na msimamizi wa Westminster.

Aidha mfalme huyo atakutana pia na wajumbe wa Baraza la Mawaziri watakaokuwa wameambatana na Waziri mkuu wa nchi hiyo, pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani.

Mfalme mpya huyo anatangazwa leo katika hafla inayofanyika katika Kasri la St. James’s jijini London.