Mgombe wa CCM Ushetu ashinda kwa kupata kura 10,335

Mbunge mteule katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Chereheni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Muktasari:

  • Msimamizi wa Uchaguzi, Mwalimu Lino Pius amesema idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 165,418 

Kahama. Mgombe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 10,335 sawa na asilimia 96.6 ya kura zote zilizopigwa jimboni hapo.

 Awali vyama vya siasa 16 vilijitokeza kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo lakini vyama 14 vilikosa sifa na baadhi yao kushindwa kurejesha fomu mpaka muda ulipokwisha huku  CCM na ACT Wazalendo vikikidhi vigezo na kugombea.

 Akitangaza matokea hayo, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Mwalimu Lino Pius amesema idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ni 165,418 lakini waliopiga kura walikuwa  107188.

 Asema kati ya kura hizo idadi halali ya kura zilizopiga zilikuwa 106,945, idadi ya kura zilizokataliwa zilikuwa kura 243, huku mgombea wa ACT Wazalendo Julius Nkwabi Mabula akipata kura 3588 sawa na asilimia 3.4.

Hata hivyo,  Mwalimu Mwageni amesema kuwa, mpaka anatangaza matokea hayo hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza katika vituo vya kupiga kura, hivyo uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na wananchi walijitokeza vile ilivyowezekana.