Mkapa alivyopanda kizimbani na kutoa ushahidi mzito kumtetea Balozi Costa Mahalu

Mkapa alivyopanda kizimbani na kutoa ushahidi mzito kumtetea Balozi Costa Mahalu

Muktasari:

  • Jana katika sehemu ya pili ya simulizi ya kesi ya aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Ricky Costa Mahalu, tuliona jinsi aliyekuwa Rais wa Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa alivyoamua kujitosa katika kesi hiyo kwa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kiapo kama kielelezo cha ushahidi wake wa utetezi.

Jana katika sehemu ya pili ya simulizi ya kesi ya aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Ricky Costa Mahalu, tuliona jinsi aliyekuwa Rais wa Tatu wa Tanzania, Hayati Benjamin Mkapa alivyoamua kujitosa katika kesi hiyo kwa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kiapo kama kielelezo cha ushahidi wake wa utetezi.

 Kesi hiyo ilipata umaarafu baada ya Rais Mkapa (wakati huo akiwa amestaafu) kuorodheshwa kama mmoja wa mashahidi watakaopanda kizimbani kumtetea Profesa Mahalu.

Wengine waliotajwa kama mashahidi wa utetezi alikuwa ni Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, John Magufuli.

Endelea Licha ya kuwasilisha kiapo chake mahakamani, Mei 7, 2012, Mkapa alilazimika kufika mahakamani mwenyewe na kusimama kizimbani kutoa ushahidi wake.

 Mmoja wa mawakili aliyekuwa akimtetea Profesa Mahalu alisema kitendo cha Mkapa kupanda kizimbani kilionyesha jinsi Rais huyo mstaafu alilivyokuwa mwaminifu na aliyeweza kusimamia kile alichokijua na kukiamini.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya ushahidi, shahidi ambaye hawezi kufika mahakamani kutokana na mazingira yoyote yale au ana kinga ya kisheria kutokufika mahakamani anaruhusiwa kutoa ushahidi wake kwa njia ya kiapo.

Mkapa alivyopanda kizimbani na kutoa ushahidi mzito kumtetea Balozi Costa Mahalu

Hata hivyo, alisema uzito wa ushahidi wa kiapo hupungua hasa pale anaposhindwa kuhojiwa na wakili wa upande pinzani kuhusu maelezo yake. Wakili Alex Mgongolwa alisema walipomfafanulia nafasi ya kiapo chake, Mkapa aliamua kwenda mahakamani mwenyewe.

Katika kitabu chake cha historia ya maisha yake -- My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu) alichokizindua Novemba 12, 2019, Mkapa anaelezea sababu ya uamuzi huo wa kwenda kusimama kizimbani. Alisema ingawa wanasiasa wengi hawakupenda achukue uamuzi huo wa kwenda kusimama kizimbani kutoa ushahidi, aliamua kufanya hivyo kwa kuwa alitaka haki itendeke.

ya muda mrefu kupita tangu alipowasilisha hati ya kiapo chake kwa lengo la kumtetea Profesa Mahalu, hatimaye ilifika siku ambayo Mkapa alipanda kizimbani yeye mwenyewe kutoa ushahidi wa mdomo.

Jumatatu, Mei 7, 2012, Mkapa aliandika rekodi ya kuwa kiongozi kwanza wa hadhi yake, mwenye kinga ya kisheria, kupanda kizimbani kutoa ushahidi, tena kumtetea mtu aliyeshtakiwa na Serikali aliyowahi kuiongoza.

Mkapa na msafara wake waliwasili mahakamani hapo saa 3:45 asubuhi akitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye rangi ya kijivu iliyokolea. Akiwa amevalia suti ya rangi ya kijivu na viatu nyeusi vya ngozi, Mkapa alishuka na kuelekea ndani ya jengo la mahakama.

Tofauti na watu wengine maarufu ambao wawapo mahakamani kwa sababu yoyote ile huwakwepa waandishi wa habari, Mkapa alionesha tabasamu alipowaona na waandishi waliokuwa wakifanya kila jitihada kupata picha nzuri.

Aliingia katika chumba maalumu cha mapumziko na kukaa humo hadi saa 5:32 alipoelekezwa kuingia mahakamani kutoa ushahidi wake.

 Kabla ya kuanza kutoa ushahidi, alikula kiapo cha ahadi ya kutoa ushahidi wa ukweli na ukweli mtupu.

Baada ya kiapo hicho alianza kutoa ushahidi huku akiongozwa na Mgongolwa na baadaye kuhojiwa na mawakili wa upande wa mashtaka kuhusi ushahidi wake aliokuwa ameutoa.

 Aliondoka katika chumba cha mahakama saa 7:31 alipomaliza kutoa ushahidi wake ambao ulivutia kutokana na aina ya maelezo na namna alivyokuwa akiyatoa.

Alijibu maswali kwa kujiamini na kwa umakini huku mara kadhaa akiwavunja mbavu wasilizaji kwa jinsi alivyokuwa akijibu maswali ya mawakili wa Serikali na yeye mwenyewe akishindwa kujizuia kucheka.

Akataa kujibu swali

Wakati akihojiwa na waendesha mashtaka Mkapa alikataa kujibu swali moja alilioulizwa akidai kuwa si kila swali anaweza kulijibu kwani kuna maswali mengine akiyajibu kiundani yanaweza kusababisha kuharibika kwa uhusianobaina ya Tanzania na nchi nyingine.

Katika ushahidi wake wa msingi, Mkapa alianza kwa kueleza hisitoaria ya utumishi wake katika nafasi za kidiplomasia, kabla ya kuingia kwenye msingi wa kesi, yaani mchakato wa ununuzi wa jengo hilo. Akielezea mchakato mzima wa ununuzi wa jengo hilo ambalo alidai Serikali yake ilifahamu ununuzi wake na tataribu za malipo baada ya kufahamishwa na Profesa Mahalu na kwamba lilinunuliwa kwa maagizo ya Serikali yake.

 Alisema mbali na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wizara nyingine zilizohusika na mchakato wa ununuzi wa jengo hilo ni Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maende[1]leo ya Makazi.

Alidai kuwa wizara hizo zote zilituma wataalamu wake kufanya uthamini wa jengo hilo kabla ya ununuzi. Akizungumzia maelezo yaliyoko katika kielelezo cha 6 cha ushahidi wa upande wa utetezi ambcho ni taarifa ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bungeni wakati huo, Jakaya Kikwete, juu ya mchakato waununuzi wa jengo hilo, Mkapa alisisitiza.

Maneno hayo ni sahihi, hayo ndiyo ninayoajua mimi kuwa ndio yaliyotokea.

Taarifa hiyo pamoja na mambo mengine inaeleza kuwa jengo hilo lilinunuliwa kwa jumla ya Sh2.9 bilioni na kwamba ingawa hati za umiliki wa jengo hilo zilishawasilishwa wizarani na kupelekwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alidai hajawahi kupata malalamiko yoyote kutoka nchiniItalia kuhusu ukiukwaji wa sheria katika mchakato wa ununuzi wa jengo hilo na wala kwa mmiliki wa jengo hilo kudai kuwa alilipwa pesa pungufu ya kiasi walichokubaliana.

Pia alikiri kuwa alitambua kuwa muuzaji alipaswa alipwe malipo kwa kutumia akaunti mbili tofauti na Serikali ilitoa baraka na kwamba yeye alitaarifiwa na hakuzuia kulipa kwa utaratibu huo. Kuhusu kuwepo kwa mikataba miwili katika ununuzi wa jengo hilo, Mkapa alijibu kuwa anachoweza kukumbuka kwa hakika ni kwamba aliambiwa kuwa kuna malipo katika akaunti mbili tofauti.

Akizungumzia mawasiliano yake na Profesa Mahalu wakati akiwa Balozi alidai kuwa walikuwa wakiwasiliana ama kwa maandishi au kwa mdomo na kwamba hiyo ilitegemea usiri wa jambo husika. Alisisitiza kuwa wakati wa mchakato wa ununuzi wa jengo hilo waliwasiliana pia.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu ushahidi wa shahidi wa kwanza upande wa mashtaka, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wake, Martin Lumbanga kuwa alikuwa hajui mchakato wa ununuzi wa jengo hilo, Mkapa, alieleza kushangazwa na taarifa hizo za ushahidi huo wa Lumbanga