Mkazi Mbagala adakwa na polisi kwa unyang’anyi

Thursday January 14 2021

Dar es Salaam. Hassan Mohammed, mkazi wa Mbagala Mchikichini jijini Dar es Salaam amekamatwa na polisi Wilaya ya Temeke kwa tuhuma za kuvunja nyumba usiku na kufanya unyang’anyi.

Akizungumza leo Alhamisi Januari 14, 2021 kamanda wa polisi wa Wilaya hiyo,  Amon Kakwale amesema baada ya kumfuatilia mtuhumiwa huyo walitambua nyumba anayoishi walimkuta na vitu mbalimbali vya wizi.

“Makachero wetu walifanya upekuzi nyumbani kwake na kukuta simu saba, hereni pea sita,  vocha 146 za mitandao mbalimbali ya kampuni za simu, laini 10 za mitandao mbalimbali, mikoba ya kinamama, visu pamoja na plaizi,” amesema Kamanda Kakwele.

Aidha amesema upelelezi dhidi ya vitendo vya unyang’anyi wa mali za wananchi unaendelea kuwatafuta watu wengine wanaohusika na vitendo hivyo.

Advertisement