Mke ashikiliwa akidaiwa kumuua mumewe kwa kisu

Muktasari:

Jeshi la Polisi   Mkoani Pwani linashikilia Mkazi wa kijiji cha Mbweni (jina limehifadhiwa) Halmahauri ya Bagamoyo Mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mume wake.

Bagamoyo. Jeshi la Polisi   Mkoani Pwani linashikilia Mkazi wa kijiji cha Mbweni (jina limehifadhiwa) Halmahauri ya Bagamoyo Mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mume wake.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Pius Lutumo leo Jumatano Septema 14, imesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo kijijini hapo.

"Mtuhumiwa alinipigia simu mumewe akimtaka arejee nyumbani mapema kwa kuwa mtoto wao anaumwa na alipoona mumewe anachelewa kurudi alimfuata baa na akakuta anamenya chungwa kutumia kisu," amesema.


Lutumo amesema, mwanamke huyo alimnyang'anya kisu mumewe na kuanza kumchoma maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Kamanda Lutumo amesema kuwa kutokana na kitendo hicho, mwili wa marehemu ulivuja damu kwa wingi na kusababisha kifo.

Amesema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Zahanati ya Mbwewe.

Ametoa wito kwa Wakazi Mkoani Pwani kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria.