Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkorea anayedaiwa kukutwa na vipande 504 vya meno, kuendelea kusota rumande

Muktasari:

  • Ra, anadaiwa kukutwa na vipande 504 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh6.4 bilioni bila kuwa na kibali.


Dar es Salaam. Mshtakiwa Un Hyok Ra (37) ambaye ni raia wa Korea Kaskazini anayekabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kumiliki vipande 504 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh6.4 bilioni, ataendelea kusalia rumande hadi Juni 23, 2026 kesi yake itakapotajwa.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Florida Wencelaus ameieleza Mahakama hiyo leo Jumanne Juni 9, 2026 wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk Salome Mshasha.

"Shauri limeitishwa kwako kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa leo hajaletwa mahakamani hapa na upande wa mashtaka bado tunaendelea na upelelezi dhidi ya mshtakiwa huyu," amedai Wencelaus na kuongeza.

"Kwa sababu hiyo, tunaomba mahakama yako itupangie tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuangalia iwapo upelelezi wake umekamilika,”amedai.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo hakupelekwa mahakamani hapo na badala yake, kesi hiyo iliahirishwa kwa njia ya video huku mshtakiwa akiwa rumande.

Hakimu Mshasha amekubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hadi Juni 23, 2026 kwa ajili ya kutajwa.

"Kwa sababu hiyo, kesi naiahirisha hadi Juni 23, 2026 kwa kutajwa," amesema Mshasha.

Kwa mara ya kwanza, Ra alifikishwa mahakamani hapo, Mei 8, 2026 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 10054 ya mwaka 2026 yenye mashtaka mawili.

Katika hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa Aprili 19, 2026 katika eneo la Hoteli ya Golden Tulip–Masaki, Wilaya ya Kinondoni, alikutwa akimiliki nyara za Serikali ambazo ni vipande 504 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh6.4 bilioni, mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori nchini.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, mshtakiwa alijihusisha na biashara ya nyara za Serikali kwa kuuza vipande 504 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh6.476 bilioni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Mshtakiwa huyo hana dhamana na yupo rumande.