Mmiliki hoteli ya kitalii ya Snowcrest afariki

Mmiliki Hotel ya kitalii ya Snowcrest afariki

Muktasari:

  • Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa hoteli kadhaa za kitalii , ikiwepo Snow crest , William Mollel amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Arusha. Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha ambaye pia ni mmiliki wa hoteli kadhaa za kitalii , ikiwepo Snow crest , William Mollel amefariki Dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Akizungumza na mwananchi Mpwa wa mfanyanyabiasha huyo,Lemburis  Sirikwa amesema Mollel amefariki Jana.

"Ni kweli Mollel ambaye ni mtoto wa dada yangu amefariki Jana baada ya kuugua kwa muda mfupi na taratibu za mazishi zinaendelea"amesema

Amesema Mollel ambaye alikuwa akifanya biashara kadhaa ikiwepo ya kuendesha hoteli za kitalii ameacha watoto watatu.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara ,Viwanda na Kilimo(TCCIA) Mkoa Arusha Walter Maeda alieleza pia kusikitishwa na kifo cha mfanyabiashara huyo.

Mollel  alinunuwa hoteli hiyo, mwaka 2014 kutoka kwa mfanyabiashara  Wilfred Tarimo, hata hivyo aliingia katika mgogoro wa kushindwa kuendesha hoteli kwa ufanisini kutokana na kurithi madeni mengi ya wazabuni na wafanyakazi.

Kwa mara ya mwisho kuzungumza na mwananchi kabla ya kifo chake  alisema alinunua hoteli hiyo kwa mkopo wa dola 8 milioni kutoka benki ya PTA na na standard chartered.

"Nilitegemea baada ya kupata mkopo wa kununua hoteli  hii niifanye ya kimataifa na kuunganisha na mtandao wa hoteli kubwa duniani''alisema.

Kifo cha Mollel kimetokea  takribani mwezi miwili tangu kifo Jacob Ombay   mmiliki mwingine wa hoteli  nane  za kitalii.

 Ombay alikuwa anamiliki hoteli za Bougainvillea safari lodge, country lodge karatu,Ngorongoro coffee lodge, lake Eyasi safari lodge,Sangaiwe tented lodge, Thorn tree camp,Hippo Traill camp.

Katibu mtendaji wa chama cha mawakala wa utalii nchini-(TATO) Sirili Akko amesema vifo vya wafanyabiashara hao ni pigo Kwa sekta ya Utalii.