Mobetto na Rayvanny wahojiwa, waachiwa

Wednesday February 17 2021
MOBETTOPICCC

Kajala Masanja

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Video ya msanii Rayvanny na Paula mitandaoni yaibua mapya. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mkali huyo wa wimbo wa Kiuno na Teamo  na mwanamitindo Hamisa Mobetto kuhojiwa polisi kwa zaidi ya saa mbili  na kisha kuachiwa.

Walifika kituo cha polisi Oysterbay jana Jumanne Februari 16, 2021 na kuhojiwa kwa zaidi ya saa mbii kuhusu tuhuma za Kajala kwamba Mobetto ndio alimpeleka binti yake kwa Rayvanny, baada ya kumuomba atoke naye kwa ajili ya chakula cha mchana

MOBETTTOPICCRAYVANN

Rayvanny

Shutuma hizo zilijibiwa na Hamisa kupitia mtandao wa Instagram ,  ambaye mbali na kukanusha kupitia mwanasheria wake alimuandikia barua Kajala kumtaka akanushe alichokisema ndani ya saa 12 kabla hajamfungulia mashtaka ya kumchafulia jina.
Akizungumza na Mwananchi Digital Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema wasanii hao walijisalimisha kituo cha Polisi Kawe, kabla ya kuhamishiwa Oysterbay kwa mahojiano zaidi.

MOBETTOPIC

“Hivi ninavyokupigia simu wanamalizia taratibu waondoke, maana wameshamaliza mahojiano, ”amesema Kingai jana saa 4:12 usiku.

Advertisement
MOBETTTOPICCCCC

Hamisa Mobetto

Kingai amefafanua kuwa wasanii hao waliachiwa baada ya kumaliza mahojiano na Polisi kujiridhisha hakuna jambo litakaloingilia ushahidi.

Advertisement