Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moshi wavalia njuga suala la usafi kuirudisha hadhi yake

Moshi. Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Bomambuzi wilayani Moshi wameamua kulivalia njuga suala la kuimarisha usafi wa mazingira katika Manispaa ya hiyo kwa  kufanya usafi katika maeneo yote ya mji huo lengo ikiwa ni kuirejesha  katika hadhi yake ya awali.


Mwaka 2022 Manispaa hiyo ilishika nafasi ya tatu ya usafi wa mazingira kutoka nafasi ya kwanza iliyokuwepo mwaka 2021.


Akizungumzia shughuli ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya kata ya Bomambuzi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kata ya Bomambuzi, Yusuf Mwakasege amesema suala la utunzaji wa mazingira lina umuhimu wake na hivyo wamepanga kila baada ya wiki moja kufanya usafi ili kuhakikisha mji huo unarudia katika hali yake ya awali.  


Amesema pamoja na Manispaa hiyo kushika nafasi ya tatu, watahakikisha mjini huo pamoja na kata hiyo inakuwa ya mfano ili maeneo mengine waweze kuja na kujifunza suala la utunzaji wa mazingira.


"Tumeamua kufanya usafi angalau kila baada ya wiki au wiki mbili katika maeneo yetu,  hivyo tutapita katika maeneo ambayo yanatolea huduma mblimbali kukahikisha tunaondoa taka zote na kuzichoma, pamoja pamoja na kutoa uchafu kwenye mitaro yote, ili tuweke maeneo yetu kuwa safi,"


"Tunataka hii kata iwe mfano, watu wengine watoke maeneo mengine kwa ajili ya kujifunza usafi, tunatekeleza ilani ya Chama chetu na tumeamua kufanya hivi kwasababu tunataka tuuweke mji wetu katika usafi," amesema Mwakasege


Ramadhani Katavo, Balozi shina namba 5, kata ya Bomambuzi, Manispaa ya Moshi amesema licha ya viongozi kulivalia njuga suala la usafi wa mazingira jamii nayo inapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha maeneo yanayowazunguka yanakuwa masafi.


"Usafi ni afya na inaweza kutuondolea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, pia tunafanya hivi kuhakisha mji wetu una rudi katika nafasi yake ya kwanza  ya usafi wa mazingira  iliyokuwepo maana sasahivi Mji wetu umeshika nafasi ya tatu,"


"Tumeamua kuboresha mazingira ya mji wetu wa Moshi na kila Jumamosi tumepanga tufanye usafi kwa kasi kutokana na kwamba tumerudi nyuma katika ile nafasi tuliyokuwa nayo kipindi cha nyuma,"amesema


Naye, Katibu wa UWT tawi la Relini, Elizabeth Kari amesema kama jumuiya wameona ni vyema kufanya usafi wa kila mara ili kuuweka mji katika hadhi yake ya usafi kwa kuwa mji wa Manispaa ya Moshi ndio lango la mkoa wa Kilimanjaro.


"Kama Jumuiya tumeamua siku ya Jumamosi tufanye usafi ili tuweke mazingira vizuri, mji wetu unatakiwa uwe safi, tumeamka kwa kasi nyingine mpya ili tuweze kurudi katika hali iliyokuwepo ya awali ya mji wetu wa Manispaa kuwa safi, "


"Kama sisi tulivyoamua kuonyesha mfano,  tunaomba wananchi wetu wajitokeze kwa wingi na kwa umoja wao bila ubaguzi kufanya usafi katika maeneo yao ili sasa mji wetu uendelee kuwa  msafi,"


Katamba Abdallah, Katibu wa Jumuiya ya wazazi tawi la Relini, Manispaa ya Moshi amesema wao kama chama wataendelea kujitolea kwa hali zote kuhakikisha mji wa Moshi unarudi katika hadhi yake.


"Wananchi wasichafue mazingira, wajitahidi wafanye usafi maana wakati mwingine mtaani uchafu unatupwa ovyo, sisi kama chama cha Mapinduzi tumefurahi kufanya zoezi hili la kujitolea na ni  zoezi ambalo litakuwa endelevu, tutakwenda hadi kwenye mashule, hospitali, haya ni majukumu yetu kama chama cha Mapinduzi," amesema Abdallah