Moto wateketeza vifaa vya wanafunzi

Moto wateketeza vifaa vya wanafunzi

Muktasari:

  • Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya  Geita kwa kushirikiana na askari wa GGM wamedhibiti moto uliowaka kwenye moja ya darasa la Shule ya sekondari Geita iliyopo mjini Geita.

 Geita. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya  Geita kwa kushirikiana na askari wa GGM wamedhibiti moto uliowaka kwenye moja ya darasa la Shule ya sekondari Geita iliyopo mjini Geita.

Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana umeanza kuwaka saa 3 usiku na kuteketeza magodoro na masanduku ya wanafunzi yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye chumba hicho.

Akizungumzia ajali hiyo mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amesema hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo lakini moto huo umeunguza kwa kiasi kikubwa magodoro na masanduku yaliyokuwa na nguo na daftari za wanafunzi.

Shimo amesema pamoja na moto huo kudhibitiwa, polisi watafanya doria kuhakikisha usalama unakuwepo katika eneo hilo na kwamba ataunda kamati kuchunguza chanzo cha moto huo.