Msaada wa Ufaransa katika malengo ya Tanzania ya usawa wa kijinsia

Wednesday July 14 2021
ufaransapic

Mwanamke ambaye ni mnufaika wa mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ufaransa akiuza bidhaa mbalimbali za kilimo.

Ufaransa ina historia ndefu ya kupigania usawa wa kijinsia, lakini Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron aliamua kuufanya usawa wa kijinsia uwe kipaumbele cha ajenda yake.

Ufaransa sasa inafanya kazi katika ngazi zote kukuza hatua hizo zilizobeba matarajio ya wengi kupitia diplomasia halisi ya kusimamia haki za mwanamke. Kwa nchini Tan-zania, pamoja na asasi za kiraia, Ufaransa kwa pamoja inafadhili miradi ya kukuza uwezeshaji wanawake kiu-chumi na kutetea usawa wa kijinsia.

Jukumu la Ufaransa kimataifa la kuwa kinara wa suala la jinsia

Miaka 26 baada ya mkutano wa wanawake uliofanyika Beijing, hakuna nchi inayoweza kudai imefanikiwa katika suala la usawa wa kijinsia. Ingawa mkutano huo ulicha-giza umuhimu wa kuzichukulia haki za wanawake kama haki za binadamu, maazimio ambayo yalifikiwa mwaka 1995 kuifanya dunia kuwa eneo salama kwa wanawake, ambapo wanawake na wanaume wanaweza kuishi sawa, suala hilo limeshindikana.

Vikwazo vya kimfumo ambavyo vimebakia vinahitajika kushughulikiwa. Kwa kushawishika kwamba wadau wote wanatakiwa kulivalia njuga suala hili, Ufaransa iliandaa kwa kushirikiana na Mexico na UN Women, Jukwaa la Usawa wa Kijinsia. Jukwaa hili la kihistoria lilifanyika Paris Juni 30 hadi Julai 2, 2021 likihudhuriwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango aliyemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan na kuonyesha wajibu wa Tanzania katika suala la usawa wa jinsia.

Jukwaa hilo lilileta pamoja Serikali mbalimbali, mashirika ya vijana, wanaharakati watetezi wa haki za wanawake, asasi za kiraia na mashirika ya kimataifa, wanaharakati na sekta binafsi ili kukuza usawa wa kijinsia. Kampeni ya Usawa wa Kijinsia ilifafanua vipaumbele 6 ambavyo ni; unyanyasaji wa kijinsia, haki ya kiuchumi, uhuru wa kutawala na haki ya afya ya uzazi na jinsia, hatua za utetezi wa haki za wanawake dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, teknolojia na uvumbuzi kwa ajili ya usawa wa kijinsia, harakati za utetezi wa haki za wanawake na uongozi.

Advertisement

Akijumuika katika Jukwaa hilo lililoonekana kushika kasi, Rais Samia alijitolea kusimamia mkakati wa kuchukua hatua dhidi ya “haki na usawa wa kiuchumi”, ili kuharakisha uwezeshaji wa wanawake kiuchumi nchini na kuhakikisha ushiriki wao wa nguvu kwa miaka mitano ijayo.

Sambamba na ahadi hiyo rasmi, Ubalozi wa Ufaransa unafadhili mradi wa kukuza uwezeshaji wanawake kiuchumi kupitia kilimo asilia nchini.

Wanaharakati wanawake wa Kitanzania dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Kwa kuwa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na kijamii na usawa wa kijinsia ni mahitaji ya msingi ya maendeleo endelevu, mipango ya maendeleo ya Ufaransa ina-jielekeza zaidi katika masuala ya kijinsia.

Nchini Tanzania, asilimia 60 ya idadi ya wanawake wanaishi katika umaskini uliokithiri, asilimia 80 ya nguvu kazi ya wakulima wadogo ni wanawake ambao wanakabiliwa na changamoto ya kupata ardhi na mikopo na kufaidika na uzalishaji wao.

Uhusishwaji wa moja kwa moja wa umaskini na wanawake ni changamoto ya kweli, hususan katika sekta ya kilimo. Mradi bunifu wa miaka 2 wa GAPE, “Uwezeshaji wa Wasichana kupitia kilimo cha ikolojia na endelevu”, ulizin-duliwa mwaka huu na Ubalozi wa Ufaransa na kupewa kiasi cha fedha cha Sh1.6 bilioni.

Mpango huu unalenga kuimarisha usawa wa kijinsia wakati huo huo unachangia ukuzaji wa kilimo cha ikolojia, kinachofahamika kitaalamu kama Agroikolojia. Agroikolojia ni kilimo endelevu, kinachozingatia mbinu za kilimo zinazoheshimu mazingira na asili. Inahifadhi bayoanuwai, maliasili na rutuba ya udongo wakati huo huo ikihakikisha usalama wa chakula.

Mafunzo ya vikundi vya wanawake katika shughuli za kilimo cha utunzaji ekolojia na mazingira na msaada katika kukuza biashara zao ndogo ni sababu halisi za hamasa na uhuru wao. Mradi huu pia unakuza ukombozi binafsi na wa kijamii wa wanawake kwa kujenga ujasiri wa wasichana na uwezo wa kusimamia na kutetea haki zao.

Kwa mradi huu, Ubalozi wa Ufaransa unafadhili asasi za kiraia 4 za Kitanzania ili kusaidia wanawake na wasichana 2,000 walio katika mazingira magumu kwa maeneo ya Dodoma, Zanzibar na Tabora. Taasisi ya Asasi ya Kiraia (FCS), Msichana Initiative (MI), Practical Permaculture Institute of Zanzibar (PPIZ) na Kilimo Endelevu Tanzania (SAT), washirika wa muda mrefu wa Ubalozi wa Ufaransa, wanafanya kazi kwa kushirikiana na kubadilishana uwezo wao katika kilimo cha utunzaji ikolojia (Agroikolojia) na uwezeshaji wa wanawake na wasichana.

Mamlaka za kitaifa na za mitaa pia zinahusishwa ili kuhamasisha wadau katika ngazi zote na kuboresha hali ya wanawake.


Advertisement