Mshikemshike wananchi kuzuiwa kuzika

Mshikemshike wananchi kuzuiwa kuzika

Muktasari:

  • Wakazi wa mtaa wa Msasani kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wamelalamikia kuzuiwa kufanya shughuli za maziko eneo ambalo walikuwa wakistiri miili ya wafu tangu mwaka 1974 kwa madai kuwa ni mali ya Jeshi.

Katavi. Wakazi wa mtaa wa Msasani kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wamelalamikia kuzuiwa kufanya shughuli za maziko eneo ambalo walikuwa wakistiri miili ya wafu tangu mwaka 1974 kwa madai kuwa ni mali ya Jeshi.

Wakizungumza na Mwananchi juzi kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi hao walisema wakati wakichimba kaburi kwa ajili ya maziko ya mwenzao walipata zuio kutoka kwa mmoja wa wanajeshi.

“Alipofika makaburini alituambia msichimbe hili ni eneo la Jeshi, diwani aliongea naye akaturuhusu akisema iwe mwanzo na mwisho, nimewaruhusu kwa kuwa mmeanza kuchimba, wakapiga na picha,” alisema Elias Said.

Ozana Nyomezi, mkazi wa Msasani alisema eneo hilo lilizinduliwa rasmi 1974 kuwa maziko na Padri William ambapo wanajeshi waliingia 1986 wakakuta linatumika na tayari watu wengi walishazikwa katika eneo hilo.

“Sehemu wanayodai ni eneo la jeshi alikuwepo mzee mmoja pale chini alifiwa na mama yake ndiyo alikuwa wa kwanza kuzikwa katika makaburi haya, nashindwa kuelewa kwamba lilikuwa eneo la jeshi, yale makaburi wameyakuta pale wamevamia,” alisema Ozana.

Diwani wa kata ya Mpandahoteli, Hamis Misigalo alisema kuwa suala hilo linawashangaza wanadhani kuna kitu nyuma ya pazia ambacho kinajulikana lakini hawafahamu kwa nini serikali imeshindwa kushughulikia.

“Nasema haya kwa sababu watu wamejenga maghala ndani ya eneo hilo, kuna TPM Redio Mpanda na wengine wanafanya kazi nyingine nyingi tu hawasumbuliwi na chochote, inasikitisha, wananchi wangu wanaumia,” alisema Jamila.

akaongeza.

“Nilibaini changamoto hiyo nikamuagiza Mkurugenzi wa Manispaa aweze kutafuta eneo lingine ambalo litatumiwa na wananchi wa Msasanina kata ya Mpandahoteli kwa ujumla kuhifadhi wapendwa wao wanaotangulia mbele za haki hivyo wavute subira ,”alisema.