Muswada wa huduma za habari hautawasilishwa Bunge hili

Msemaji Kuu wa Serikali, Garson Msigwa

What you need to know:

  • Serikali imesema haitawasilisha bungeni miswada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali ukiwamo muswada wa huduma za habari.

Dodoma. Serikali imetanga kutowasilisha muswada wa huduma za habari namba 12 wa mwaka 2016, baada ya kukosa nafasi.

 Mbali na miswada hiyo, Serikali imesema muswada wa Bima ya Afya kwa wote utawasilishwa kwenye Bunge hili la 10 ambalo ni mahususi kupokea taarifa mbalimbali za kamati za Bunge.

Akizunguma leo Jumanne Februari 7, 2023 Msemaji Kuu wa Serikali, Garson Msigwa amesema muswada huo wa huduma za habari hakupata nafasi katika Bunge hili.

"Muswada huu na miswada mibgine sasa itawasilishwa Bunge lijalo," amesema Msigwa.

Amesema ratiba za Bunge hili lenye mikutano 10 imebana kiasi cha kukosa nafasi kwa miswada mingine ukiwamo wa muswada wa huduma za habari.

"Lile jambo letu ambalo mmekuwa mkiuliza, mchakato wake ulikuwa umekamilika, maoni ya wadau yamekamilika, tatizo ni nafasi," amesema.

Akijibu swali kuhusu muswada wa Bima ya Afya amesema huo utawasilishwa katika Bunge hili.

Msigwa amesema Watanzania wanasubiri kwa hamu kuhusu muswada huo na Serikali haiwezi kuwaamgusha.