Mvua yaleta maafa Tabora, yaua watatu

Friday November 26 2021
MVUA PIC

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao. Picha na Robert Kakwesi

By Robert Kakwesi

Tabora. Mvua zilizoanza kunyesha katika baadhi ya maeneo mkoani Tabora zisababisha vifo vya watu watatu akiwamo mtoto wa mwaka mmoja.

Watu hao wamefariki baada ya mvua iliyoambatana na radi kuunguza nyumba waliokuwemo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea Novemba 25, 2021 katika kitongoji cha Mkuyuni, Kijiji cha Lumbulasiasa kata ya Ugunga Wilaya ya Kaliua.

Amesema wakati mvua inanyesha, radi radi ilipiga na kuiunguza nyumba ambayo walikuwemo.

Amewataja waliofariki kuwa ni John Matelemki (48), Mbisi Maziku (28) na mtoto wa mwaka mmoja, Raphael John.

Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua ambazo zimeanza kunyesha katika baadhi ya ya mkoa huo.

Advertisement

"Tunawataka wananchi kuhakikisha Wanaochukua tahadhari wasije kudhurika na mvua hizi zinazonyesha kipindi hiki"amesema

Mwisho.

Advertisement