Mwandishi wa habari afariki dunia

Marehemu Amina Hasani enzi za uhai wake alipokuwa akitekeleza majuku yake ya kuhabarisha watu.

Muktasari:

  • Kifo cha mwandishi wa habari wa Redio Sengerema Amina Hassan aliyefariki Septermba 11 mwaka huu baada ya kugua kwa muda mfupi, kimeleta simanzi na majonzi makubwa kwa familia ya habari na W anasengerema kwa ujumla.

Sengerema. Mwandishi wa habari wa Redio Sengerema, Amina Hasan amefariki dunia jana Septemba 11, katika zahanati ya Mama alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kugua kwa muda mfupi.


Afisa habari Wilaya ya Sengerema, Silvanus Mdalami amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambacho kimeleta simanza na majonzi makubwa kwa familia ya habari wilayani humo.


Marehemu Amini Hassan atakumbukwa na wanasengerema kutokana na umahiri wake wa kutangaza kipindi cha Safari Mseto, mawaidha ya dini ya Kiislamu pamoja na mziki wa taarabu.

Marehemu alijiunga na Redio Sengerema toka mwaka 2017 na ameacha mume na mtoto mmoja. Anatarajia kusafirishwa kuelekea Kanyanga Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera kwa ajili ya maziko.


Mmoja wa waandishi waliofanya kazi na marehemu, Tumaini John amesema marehemu Amina alikuwa mcheshi na mtu mwenye hofu ya Mungu na alikuwa anapenda ushirikiano wakati anatekeleza majukumu yake.


Naye Sospeter Butungo ambaye ni mkazi wa Sengerema amesema kifo cha Amani kimeacha pengo kwa wasikilizaji wa Redio Sengerema na atakumbukwa kwa mazuri aliyofanya enzi za uhai wake.