Mwandishi wa habari Vedasto Msungu afariki dunia

New Content Item (2)
New Content Item (2)

Muktasari:

  • Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV mkoani Morogoro, Vedasto Msungu amefariki dunia leo jioni Jumatano Februari 17, 2021 katika hospitali ya rufaa Mkoa huo.

Morogoro. Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV mkoani Morogoro, Vedasto Msungu amefariki dunia leo jioni Jumatano Februari 17, 2021 katika hospitali ya rufaa Mkoa huo.

Alilazwa katika hospitali hiyo jana Jumanne Februari 16, 2021 baada ya kupata tatizo la upumuaji.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amethibitisha kifo hicho.