Mwenge ‘kunusa’ kila halmashauri maagizo 15 ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa mkimbiza mwenge kitaifa Abdallah Kaim Mkoa wa Kaskazini Pemba Zanzibar ambao utakimbizwa katika Mikoa 31 ya Tanzania bara na visiwani katika Halmashauri 195. Picha Florence Sanawa

Muktasari:

  • Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutelekeza maagizo 15 aliyoyatoa Waziri Mkuu June mwaka jana wakati akizindua siku ya mazingira ambapo wakimbiza Mwenge kitaifa watapita katika miradi hiyo na kuangalia namna maagizo hayo yalivyotekelezwa.

Mtwara. Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa maeneo mengi ya nchi yameathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kuzitaka halmashauri kutekeleza maagizo hayo kwa ustawi wa jamii.

Kati ya maagizo hayo 15 ikiwemo Wizara ya fedha na mipango mpango kabambe wa usimazi na uhifadhi wa mazingira unakuwa kipaumbele cha bajeti kwa miaka 10, wizara, sekta na halmashauri zote nchini mpango kabambe wa uhifadhi wa mazingira unajumuishwa kwenye bajeti zao, kila halmashauri kuhakikisha maeneo yaliyoharibiwa yarejeshwa kwa kupandwa miti, mashirika yanayotumia miti na mkaa yaanze kutumia nishati mbadala iikiwemo vyuo shule na majeshi. 

Akizungumza leo Aprili Mosi, 2023 wakati akizindua mbio za mwenge kitaifa zilizofanyikia mkoani Mtwara,  alisema kuwa mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira asilimia 95 ni matokeo ya kibinadamu kwa upande mwingine dunia kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi za uharibifu wa mazingira zinazochangiwa na shughuli za kibinadamu siyo endelevu.

Alisema kuwa mabadiliko hayo yameathiri uharibifu wa ardhi, upotevu wa makazi ya wanayamapori na bainuai, uhaba wa maji safi kwa watu, usimamizi hafifu wa taka. Pia uharibifu wa misitu mabadiliko ya tabia nchi uchafuzi wa mazingira usimamizi hafifu wa kemikali   na uharbifu wa mifumo ya ekolojia ya majini ambayo yanaharibu mwelekeo wetu changamoto hizi za asili huifadhi ya mazingira ustawi wa jamii na uchumi kwa ujumla,” amesema

“Tanzania imeathirwa na uharibifu wa mazingira ambao unasababishwa mabadiliko ya tabia nchi uvamizi wa maeneo tengefu vyanzo vya maji matumzi ya kemikali mbolea na viuatilifu ufugaji wa kuhama ambao unajumuisha makundi makubwa ya wanyama,” amefafanua.

“Sambamba na hilo pia ukataji miti kwa ajili ya kuni uchomaji misitu na mikaa na mbuga. Uchimbani wa madini usiokuwa endelevu na uvunaji haramu wa mikoko na eneo kwa viumbe vamizi ndio maeneo yanayoharibu mazingira yetu,” amesema.

“Serikali itaendelea kulinda mazingira na vyanzo vya maji ambapo katika sheria ya usimamizi wa mazingira sura ya 191 ambayo imeweka masharti yanayozuia uharibifu na uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za kijamii hatua zinalenga uhifadhi endelevu wa mazingira na kuifanya dunia na nchi kuwa sehemu bora ya kuishi,” amesema

"Nakumbuka Juni mwaka jana nilitoa maagizo 15 wakati nikizindua siku ya mazingira Mkoa wa Dodoma ambapo naamini mbio za Mwenge zitapita na kuangalia utekelezaji wa maagizo hayo,” alisema Waziri Kassimu.