Mwenge wazindua Makao makuu ya Enduimet WMA

Muktasari:

  •  Mwenge wa Uhuru, umezindua mradi wa majengo ya Makao Makuu ya Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Enduimet (WMA), wilayani Longido wenye thamani ya Sh651.7 milioni


Longido. Mwenge wa Uhuru, umezindua mradi wa majengo ya Makao Makuu ya Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Enduimet (WMA), wilayani Longido wenye thamani ya Sh651.7 milioni

Mradi huo ambao sasa utawezesha WMA kuwa na kituo cha taarifa za watalii umejengwa na Taasisi ya jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Kwa ufadhili wa shirika la uhifadhi la kimataifa (WWF-TCO).

Kiongozi wa mbio za mwenge, Sahili Geraruma ameipongeza TNRF na WMA kutekeleza mradi huo ambao wenye lengo la kukuza utalii nchini.

Geraruma ameitaka WMA kutunza majengo hayo ili yatumike Kwa muda mrefu zaidi kusaidia sekta ya Utalii nchini.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa mradi huo, Mkurugenzi wa TNRF, Zakaria Faustin ameishukuru  Serikali Kwa kutambua mchango na jitihada zao za kuendeleza uhifadhi nchini.

"Mradi huu ni sehemu tu ya miradi ya TNRF ambayo tunaifanya nchini katika maeneo mbalimbali ili kuendeleza uhifadhi Kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo"amesema.