Mwili wa aliyejiua baada ya kumuua mkewe kwa risasi wachukuliwa mochwari

Wednesday June 01 2022
mwili pic

Ndugu wa Said Oswayo wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili Said ambaye alijiua kwa kujipiga risasi baada ya kumuua mkewe Swalha Salum. Picha na Mgongo Kaitira

By Mgongo Kaitira

Mwanza. Baadhi ya ndugu na waombolezaji wamejitokeza kuchukua jeneza lenye mwili wa mkazi wa Buswelu, Said Oswayo aliyejiua kwa kujipiga risasi baada ya kumuua mkewe, Swalha Salum kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

ajiua pic

Oswayo anadaiwa kumuua mkewe kwa kumfyafulia risasi saba Mei 28,2022 kisha kutoweka nyumbani kwake huku mwili wake ukipatika Jumatatu Mei 30,2022 jioni ukielea ndani ya Ziwa Victoria katija ufukwe wa Rock Beach.

risasi pic

Picha ya Swalha Salum aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mmewe, Said Oswayo jijini Mwanza

Mwili huo umchukuliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando na kusindikizwa na ndugu zake na wale wa upande wa mke wake.

Wakati mwili wa mkewe ukizikwa jana Mei 31, 2022 katika makaburi yaliyopo Kirumba mkoani hapa, mwili wa Said utapelekwa nyumbani kwake mtaa wa Mbogamboga kata ya Buswelu wilayani Ilemela mkoani Mwanza kabla ya kusafirishwa kwenda kijiji cha Etaro kilichopo wilaya ya Musoma mkoani Mara kwa ajili ya maziko.

Advertisement


Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia Mwananchi

Advertisement