Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa Balozi Mushy waagwa Handeni

Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy. Picha na Rajabu Athumani

Muktasari:

  • Balozi Celestine Mushy alifariki Desemba 13, 2022 katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori la mizigo na kuungua moto akiwa ndani.

Handeni. Mwili wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy aliyefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Tengwe kata ya Mkata Wilayani Handeni mkoa wa Tanga Desemba 13, umeagwa mjini Handeni leo Jumamosi Desemba 17, 2022.

Mwili huo umeagwa na baadhi ya viongozi wa dini na serikali kwenye ibada maalumu kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi.

Balozi Celestine Mushy alifariki Desemba 13, 2022 katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa Tanga baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori la mizigo na kuungua moto akiwa ndani.

Jana akizungumzia na Mwananchi kuhusu utaratibu wa mazishi, msemaji wa familia, Dk Kenneth Lema amesema Balozi Mushy atazikwa Jumanne ijayo nyumbani kwake, Kibosho Road, Moshi.


Viongozi wafika nyumbani kwa Balozi Mushy


Viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu wamefika nyumbani kwa Balozi Mushy kusaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa mjane wa marehemu.

Mbali na Mkuu wa Mkoa, viongozi wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa huu, Willey Machumu, wakuu wa wilaya  pamoja na wabunge wa mkoa huo ambapo wamekutana na familia na kuwafariji wafiwa pamoja na kupata ratiba na maandalizi ya maziko.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hata hivyo, vikao vya kifamilia vya taratibu za mazishi vinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Balozi Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari 2022 na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Imeandikwa na Rajab Athuman (Handeni), Janeth Joseph na Florah Temba (Moshi)