Mwili wa Mngereza wa Basata kuagwa Dar Jumanne

Saturday December 26 2020
muingerezapic

Geofrey Mngereza

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Mwili wa aliyekuwa katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),  Godfrey Mngereza utawasili  Dar es Salaam Jumatatu Desemba 28, 2020.

Taarifa iliyotolewa na Basata inaeleza kuwa mwili utaagwa Jumanne ukumbi wa Karimjee na mazishi yatafanyika Desemba 30, 2020 kijijini kwao Suji wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Inaeleza kuwakwa sasa msiba upo nyumbani kwa marehemu Kibamba Luguruni jijini Dar es Salaam.

Mngereza  alifikishws  hospitali ya rufaa Dodoma baada ya kuzidiziwa.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Ernest Ibenzi amesema tangu afikishwe hospitali Desemba 22 hali yake haikuwa nzuri jambo liliwalazimu kumuweka chumba cha uangalizi wa Katibu(ICU) na alifariki dunia akiwa katika chumba hicho.

Advertisement