Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndugu washindwa kujizuia wakiaga miili 12 Rombo

Ndugu wa waliofariki katika ajali mkoani Tanga wakishindwa kujizuia baada ya kuona miili ya ndugu zao ikiwa kwenye majeneza katika viwanja vya Hospitali ya Huruma iliyopo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro. Picha na Janeth Joseph

Rombo. Ndugu, jamaa na marafiki waliofika kuaga miili ya wapendwa wao katika viwanja vya Hospitali ya Huruma iliyopo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, wameshindwa kujizuia na baadhi kuzimia baada ya kuona miili ya ndugu Yao ikiwa  kwenye majeneza.

Ajali hiyo ilitokea Februari 4,  katika eneo la Magira Gereza, Kata ya Magira Gereza, wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko na kusababisha vifo vya watu 21 mpaka sasa.

Ndugu hao pamoja na majirani walikuwa  wakisindikiza mwili wa ndugu yao, Athanas Mrema (59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutokea jijini Dar es Salaam kuja mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko ndipo walipata ajali hiyo.

Katika mazishi ambayo yanafanyika leo, ipo familia moja ambayo inazika watu watano kwa wakati mmoja, familia nyingine wawili pamoja na wengine ambao wanazikwa mwili mmoja mmoja.

Katika viwanja hivi ipo miili 12 ambayo inaagwa leo kwa ajili ya maziko ambayo yanafanyika katika familia iliyopoteza watu 14 katika ajali hiyo.