Necta yafuta ada za mitihani shule za Serikali

Muktasari:

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Necta, wanafunzi watakaolazimika kulipa ada ya mitihani ni watahiniwa kutoka shule binafsi pekee.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limefuta ada ya mitihani kwa watahiniwa wa darasa la saba, kidato cha nne na sita kwa shule za Serikali.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Necta, wanafunzi watakaolazimika kulipa ada ya mitihani ni watahiniwa kutoka shule binafsi pekee.

“Baraza la Mitihani la Tanzania linawajulisha watu wote kuwa ada ya mtihani kwa watahiniwa wa darasa la saba, kidato cha ne na sita wa shule za Serikali imefutwa.

“Wanaotakiwa kulipa ada ya mtihani ni watahiniwa wa shule binafsi tu,” imeeleza taarifa hiyo

Msemaji wa Necta, John Nchimbi akizungumza na Mwananchi Digital amesema, ada hiyo ilikuwa Sh50, 000.