NIMR yapewa ushauri kuhusu dawa wanazozizalisha

NIMR yapewa ushauri kuhusu dawa wanazozizalisha

Muktasari:

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa wito kwa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) kufanya utafiti wa kina kwenye dawa  wanazozizalisha ili kubaini kama zimeleta tija kutibu maradhi mbalimbali.

Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge ametoa wito kwa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) kufanya utafiti wa kina kwenye dawa  wanazozizalisha ili kubaini kama zimeleta tija kutibu maradhi mbalimbali.

Ameeleza hayo jana Ijumaa Novemba 27, 2020 jijini Dodoma katika maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo nchini Tanzania katika hotuba yake iliyosomwa na mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dk Suleiman Serera

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua namna dawa wanazozizalisha zimeleta tija.

Amesema Serikali inalenga zaidi kuimarisha miundombinu ya utoaji huduma za afya ya binadamu kwa lengo la kuwezesha kila Mtanzania awe na afya bora.

Ameitaka NIMR kujikita zaidi na tafiti zinazohusu magonjwa yanayowakabili Watanzania ili wawaelimishe kujikinga na kuyaepuka kuliko kusubiri tiba na hatimaye kutekeleza malengo ya Serikali ipasavyo.

Katika maadhimisho hayo Wananchi wa Jiji la Dodoma walijitokeza kwa wingi katika shughuli ya kuchangia damu na kuchunguzwa afya zao bure.