Odinga aongoza kura za Diaspora Rwanda

Muktasari:

Raila Odinga mgombea wa Azimio la Umoja amefungua vema ukurasa wa matokeo ya uchaguzi kwa diaspora akipata kura 150, Rwanda ikilinganishwa na 81 za William Ruto.

Nairobi. Mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ameongoza katika kura zilizopigwa na Wakenya wanaoishi nchini Rwanda, akipata 150 sawa na asilimia 62.7 ikilinganishwa na 81 alizopata Ruto.

Katika taifa hilo, wagombea wengine George Wajackoyah wa Chama cha Roots na David Waihiga wa Agano wamepata kura nne kila mmoja.

Rwanda ni miongoni mwa mataifa 12 ambayo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imefungua vituo vya kupigia kura kwa raia wao wanaoishi huko.

Kwa sasa tume hiyo inaendelea kupokea matokeo ya kura kutoka kwa diaspora, huku ushindani ukionekana zaidi kwa manguli wawili wa siasa, Ruto na Odinga.

Hata hivyo, IEBC inatarajia kutangaza matokeo ya jumla ya uchaguzi huo ndani ya siku saba.