Ofisi ya Makamu wa Rais yaeleza sababu ya kutumia Suma JKT katika ujenzi

Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mary Maganga

Muktasari:

  • Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mary Maganga ametaja sababu za ofisi ya wizara hiyo kujengwa na taasisi za Serikali akisema ni unyeti wa ofisi hizo.


Dodoma. Katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mary Maganga ametaja sababu za ofisi ya wizara hiyo kujengwa na taasisi za Serikali akisema ni unyeti wa ofisi hizo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 13, 2021 wakati akisaini mkataba wa ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba.

Majengo hayo yanajengwa kwa mtindo wa Magorofa ikiwa ni awamu pili ya ujenzia ambapo Suma JKT imesaini kandarasi ya Sh18 bilioni kwa ajili ya ujenzi.

"Ujue Ofisi yatu ni ya pili kwa ukubwa na ukubwa na unyeti hivyo baadhi ya vitu huwezi kuruhusu usimamizi wa nje ndiyo maana tunachuju Suma JKT na mshauri wake ni shirika la nyumba (NHC)," amesema Maganga.

Licha ya mkataba huo kutaka jengo hilo lijengwe kwa muda usiozidi miezi 24, kiongozi huyo ameomba wajenge hata chini ya muda huo.

Amesema watumishi wengi wamepanga majengo mjini kwa sababu ya ufinyu wa ofisi walizonazo eneo la Mtumba ambako ameeleza ujenzi unakwenda kumaliza matatizo hayo.