Ondoa vinyweleo mwilini kwa nta ya sukari

Ondoa vinyweleo mwilini kwa nta ya sukari

Muktasari:

  • Vinyweleo siyo tatizo la kiafya, lakini baadhi wanawake wengi huwa vinawakwaza.

Vinyweleo siyo tatizo la kiafya, lakini baadhi wanawake wengi huwa vinawakwaza.

Ingawa kuna ambao wakiwa navyo huwaongezea mvuto wa miguu yao, lakini baadhi kama nilivyosema hawavipendi.

Kwa wanawake ambao wanavyo na wanataka kuviondoa kuna njia nzuri na rahisi ya asili ambayo wakiitumia vitaondoka na hawatapata madhara.

Unaweza kutumia nta ya sukari kuviondoa. Changanya sukari yoyote uliyonayo kikombe kimoja cha chai, maji vijiko viwili vya chakula, juisi ya limao kijiko kimoja na nusu cha chakula, chumvi kijiko kimoja cha chai, kisha bandika jikoni. Acha mchanganyiko huo uchemke hadi ubadilike kuwa rangi ya kahawia.

Endelea kuukoroga taratibu ili sukari yote iyeyuke na uwe ni rojo zito iipue na uiache kwa dakika chache ipoe.

Ikishapoa pakaa katika maeneo yenye vinyweleo kama miguuni au mikononi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni. Fanya hivyo mpaka nywele zitakapoacha kuota kwa wingi eneo husika.

Huu mchanganyiko uanitwa nta, hivyo uhifadhi katika jokofu.